God
Mistari inayomtaja God
Funika nyuso zao kwa aibu ili watu walitafute jina lako, Ee Bwana.
Hebu wajue kwamba wewe, ambaye jina lako ni Bwana, kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote.
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya wana wa Kora. Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, makao yako yapendeza kama nini!
Nafsi yangu inatamani sana, naam, hata kuona shauku, kwa ajili ya nyua za Bwana; moyo wangu na mwili wangu vinamlilia Mungu Aliye Hai.
Hata shomoro amejipatia makao, mbayuwayu amejipatia kiota mahali awezapo kuweka makinda yake: mahali karibu na madhabahu yako, Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mfalme wangu na Mungu wangu.
Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, wanaokusifu wewe daima.
Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako, na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao.
Huendelea toka nguvu hadi nguvu, hadi kila mmoja afikapo mbele za Mungu huko Sayuni.
Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu; nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo.
Ee Mungu, uitazame ngao yetu, mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako.
Siku moja katika nyua zako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu kuliko kukaa katika mahema ya waovu.
Kwa kuwa Bwana ni jua na ngao, Bwana hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia.
Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Ee Bwana, ulionyesha wema kwa nchi yako. Ulimrejeshea Yakobo baraka zake.
Ulisamehe uovu wa watu wako, na kufunika dhambi zao zote.
Uliweka kando ghadhabu yako yote na umegeuka na kuiacha hasira yako kali.
Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena, nawe uiondoe chuki yako juu yetu.
Je, utatukasirikia milele? Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote?
Je, hutatuhuisha tena, ili watu wako wakufurahie?
Utuonyeshe upendo wako usiokoma, Ee Bwana, utupe wokovu wako.
Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana; anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake: lakini nao wasirudie upumbavu.
Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao, ili utukufu wake udumu katika nchi yetu.
Naam, hakika Bwana atatoa kilicho chema, nayo nchi yetu itazaa mavuno yake.
Haki itatangulia mbele yake na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake.
Maombi ya Daudi. Ee Bwana, sikia na unijibu, kwa maana mimi ni maskini na mhitaji.