Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Umenitenga na rafiki zangu wa karibu na kunifanya chukizo kwao. Nimezuiliwa, wala siwezi kutoroka;

  2. nuru ya macho yangu imefifia kwa ajili ya huzuni. Ee Bwana, ninakuita kila siku, ninakunyooshea wewe mikono yangu.

  3. Je, wewe huwaonyesha wafu maajabu yako? Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu?

  4. Je, upendo wako hutangazwa kaburini, uaminifu wako katika Uharibifu?

  5. Je, maajabu yako hujulikana mahali pa giza, au matendo yako ya haki katika nchi ya usahaulifu?

  6. Lakini ninakulilia wewe, Ee Bwana, unisaidie; asubuhi maombi yangu huja mbele zako.

  7. Ee Bwana, kwa nini unanikataa na kunificha uso wako?

  8. Tangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo; nimepatwa na hofu zako, nami nimekata tamaa.

  9. Ghadhabu yako imepita juu yangu; hofu zako zimeniangamiza.

  10. Umeniondolea marafiki na wapendwa wangu; giza limekuwa ndilo rafiki yangu wa karibu kuliko wote.

  11. Utenzi wa Ethani Mwezrahi. Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele; kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako ujulikane kwa vizazi vyote.

  12. Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni.

  13. Ulisema, “Nimefanya agano na mteule wangu, nimemwapia mtumishi wangu Daudi,

  14. ‘Nitaimarisha uzao wako milele na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’ ”

  15. Ee Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako, uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu.

  16. Kwa kuwa ni nani katika mbingu anayeweza kulinganishwa na Bwana? Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni aliye kama Bwana?

  17. Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana, anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka.

  18. Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, ni nani aliye kama wewe? Ee Bwana, wewe ni mwenye nguvu, na uaminifu wako unakuzunguka.

  19. Wewe unatawala bahari yenye msukosuko; wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza.

  20. Wewe ulimponda Rahabu kama mmojawapo wa waliochinjwa; kwa mkono wako wenye nguvu, uliwatawanya adui zako.

  21. Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako, uliuwekea ulimwengu msingi pamoja na vyote vilivyomo.

  22. Uliumba kaskazini na kusini; Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha.

  23. Mkono wako umejaa uwezo; mkono wako una nguvu, mkono wako wa kuume umetukuzwa.

  24. Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi; upendo na uaminifu vinakutangulia.

  25. Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe, wanaotembea katika mwanga wa uwepo wako, Ee Bwana.