Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Natamani kukaa hemani mwako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.

  2. Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu, umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako.

  3. Yeye na atawazwe kwenye kiti cha enzi mbele za Mungu milele; amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde.

  4. Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.

  5. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi. Kwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko; wokovu wangu watoka kwake.

  6. Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe.

  7. Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake, tumaini langu latoka kwake.

  8. Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; ndiye ngome yangu, sitatikisika.

  9. Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu, ndiye mwamba wangu wenye nguvu na kimbilio langu.

  10. Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote, miminieni mioyo yenu kwake, kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.

  11. Jambo moja Mungu amelisema, mambo mawili nimeyasikia: kwamba, Ee Mungu, wewe una nguvu,

  12. na kwamba, Ee Bwana, wewe ni mwenye upendo. Hakika utampa kila mtu thawabu kwa kadiri ya alivyotenda.

  13. Zaburi ya Daudi. Wakati alipokuwa katika Jangwa la Yuda. Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, nakutafuta kwa moyo wote; nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu unakuonea wewe shauku, katika nchi kame na iliyochoka mahali ambapo hapana maji.

  14. Nimekuona katika mahali patakatifu na kuuona uwezo wako na utukufu wako.

  15. Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakuadhimisha.

  16. Nitakusifu siku zote za maisha yangu, na kwa jina lako nitainua mikono yangu.

  17. Nafsi yangu itatoshelezwa kama kwa wingi wa vyakula; kwa midomo iimbayo kinywa changu kitakusifu wewe.

  18. Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe, ninawaza juu yako makesha yote ya usiku.

  19. Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu, chini ya uvuli wa mbawa zako naimba.

  20. Nafsi yangu inaambatana nawe, mkono wako wa kuume hunishika.

  21. Bali mfalme atafurahi katika Mungu, wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu, bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa.

  22. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Mungu, unisikie ninapoeleza lalamiko langu, uyahifadhi maisha yangu kutokana na vitisho vya adui.

  23. Bali Mungu atawapiga kwa mishale, nao ghafula wataangushwa.

  24. Wanadamu wote wataogopa, watatangaza kazi za Mungu na kutafakari yale aliyoyatenda.

  25. Wenye haki na wafurahi katika Bwana, na wakimbilie kwake; wanyofu wote wa moyo na wamsifu yeye!