- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
Mithali10
Listen to this chapter
0:00
0:00
Njia ya Mwana Mwenye Hekima na Mwana Mpumbavu
1
Mithali za Solomoni: Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake.
2
Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini.
3
Bwana hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu.
4
Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono yenye bidii huleta utajiri.
5
Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi ni mwana mwenye hekima, lakini yeye alalaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
6
Baraka huwa taji kichwani mwa mwenye haki, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu.
7
Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka, lakini jina la mwovu litaoza.
Hekima na Nidhamu ya Maneno
8
Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo, lakini mpumbavu apayukaye huangamia.
9
Mtu mwadilifu hutembea salama, lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.
10
Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni, naye mpumbavu apayukaye huangamia.
11
Kinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uzima, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu.
12
Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote.
13
Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua, lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu.
14
Wenye hekima huhifadhi maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi.
Utajiri, Bidii na Usalama wa Kudumu
15
Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, bali ufukara ni maangamizi ya maskini.
16
Ujira wa wenye haki huwaletea uzima, lakini mapato ya waovu huwaletea adhabu.
17
Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima, lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine.
18
Yeye afichaye chuki yake ana midomo ya uongo, na yeyote anayeeneza uchonganishi ni mpumbavu.
19
Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani, lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara.
20
Ulimi wa mwenye haki ni fedha iliyo bora, bali moyo wa mwovu una thamani ndogo.
21
Midomo ya mwenye haki hulisha wengi, lakini wapumbavu hufa kwa kukosa ufahamu.
Baraka za BWANA na Hukumu ya Mwisho
22
Baraka ya Bwana hutajirisha, wala haichanganyi huzuni.
23
Mpumbavu hufurahia tabia mbaya, lakini mtu mwenye ufahamu hupendezwa na hekima.
24
Kile anachoogopa mwovu ndicho kitakachompata; kile anachoonea shauku mwenye haki atapewa.
25
Tufani inapopita, waovu hutoweka, lakini wenye haki husimama imara milele.
26
Kama siki ilivyo kwa meno na moshi kwa macho, ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma.
27
Kumcha Bwana huongeza urefu wa maisha, lakini miaka ya mwovu inafupishwa.
28
Tarajio la mwenye haki ni furaha, bali matumaini ya mwovu huwa si kitu.
29
Njia ya Bwana ni kimbilio kwa wenye haki, lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya.
30
Kamwe wenye haki hawataondolewa, bali waovu hawatasalia katika nchi.
31
Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima, bali ulimi wa upotovu utakatwa.
32
Midomo ya wenye haki inajua kile kinachofaa, bali kinywa cha mwovu hujua kile kilichopotoka tu.
Use ← → arrow keys to navigate
Settings
Reading Style
Typeface
Font Size px
Reading Width chars
Options
Study Note