- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
Ayubu27
Listen to this chapter
0:00
0:00
Mfano wa mwisho wa Ayubu waanza
1
Ndipo Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:
2
“Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu, Mwenyezi ambaye amenifanya nionje uchungu wa nafsi,
3
kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu, nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu,
4
midomo yangu haitanena uovu, wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
Kiapo cha uadilifu
5
Sitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi; hadi nife, sitakana uadilifu wangu.
6
Nitadumisha haki yangu wala sitaiacha; dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi.
7
“Watesi wangu wawe kama waovu, nao adui zangu wawe kama wasio haki!
8
Kwa maana mtu asiyemcha Mungu analo tegemeo gani anapokatiliwa mbali, Mungu anapouondoa uhai wake?
9
Je, Mungu husikiliza kilio chake, shida zimjiapo?
10
Je, anaweza kumfurahia Mwenyezi? Je, atamwita Mungu nyakati zote?
11
“Nitawafundisha juu ya uweza wa Mungu; njia za Mwenyezi sitazificha.
12
Ninyi nyote mmeona hili wenyewe. Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana?
Fungu la waovu
13
“Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu, urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi:
14
Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani, fungu lao ni kuuawa kwa upanga; wazao wake hawatakuwa kamwe na chakula cha kuwatosha.
15
Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, nao wajane wao hawatawaombolezea.
16
Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,
17
yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.
18
Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, kama kibanda alichotengeneza mlinzi.
19
Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; afunguapo macho yake, yote yametoweka.
20
Vitisho humjia kama mafuriko; dhoruba humkumba ghafula usiku.
21
Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; humzoa kutoka mahali pake.
22
Humvurumisha bila huruma, huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake.
23
Upepo humpigia makofi kwa dharau, na kumfukuza atoke mahali pake.
Use ← → arrow keys to navigate
Settings
Reading Style
Typeface
Font Size px
Reading Width chars
Options
Study Note