- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
Wagalatia5
Listen to this chapter
0:00
0:00
Simameni Imara Katika Uhuru wa Kikristo
1
Kristo alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na kongwa la utumwa.
2
Sikilizeni! Mimi, Paulo, nawaambieni kwamba kama mkikubali kutahiriwa, basi Kristo hatawafaidia chochote.
3
Namshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria yote.
4
Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu.
5
Kwa maana, kwa njia ya Roho kwa imani, tunangojea kwa shauku tumaini la haki.
6
Kwa maana ndani ya Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.
Onyo Dhidi ya Kushawishiwa kwa Uongo
7
Mlikuwa mkipiga mbio vizuri. Ni nani aliyewazuia msiitii kweli?
8
Ushawishi wa namna hiyo haukutokana na yule anayewaita.
9
“Chachu kidogo huchachua donge zima.”
10
Nina hakika katika Bwana kwamba hamtakuwa na msimamo mwingine. Mtu anayewachanganya anastahili adhabu, hata awe nani.
11
Lakini ndugu zangu, kama mimi bado ninahubiri kuhusu kutahiriwa, kwa nini bado ninateswa? Katika hiyo hali basi, kwazo la msalaba limeondolewa.
12
Laiti hao wanaowavuruga wangejihasi wao wenyewe!
Uhuru Katika Kristo
13
Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili mwe huru, hivyo msitumie uhuru wenu kama fursa ya kufuata tamaa za mwili, bali tumikianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo.
14
Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”
15
Kama mkiumana na kutafunana, angalieni, msije mkaangamizana.
Enendeni Kwa Roho
16
Kwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
17
Kwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, naye Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka.
18
Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko chini ya sheria.
Matendo ya Mwili
19
Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi,
20
kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21
husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi Ufalme wa Mungu.
Matunda ya Roho
22
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23
upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria.
24
Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili na shauku zake pamoja na tamaa zake.
25
Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, basi, tuenende kwa Roho.
26
Tusijisifu bure, tukichokozana na kuoneana wivu.
Use ← → arrow keys to navigate
Settings
Reading Style
Typeface
Font Size px
Options
Study Note