Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Vanity

88 mistari · 60 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mlionyeshwa mambo haya ili mpate kujua kuwa Bwana ndiye Mungu; hakuna mwingine ila yeye.

  2. Walizikataa amri zake, na agano alilokuwa amelifanya na baba zao, na maonyo aliyokuwa amewapa. Wakafuata sanamu zisizofaa, nao wenyewe wakawa hawafai. Wakayaiga mataifa yaliyowazunguka, ingawa Bwana alikuwa amewaonya akiwaambia, “Msifanye kama wanavyofanya,” nao wakafanya mambo ambayo Bwana alikuwa amewakataza wasifanye.

  3. Ninayachukia maisha yangu; nisingetamani kuendelea kuishi. Niache; siku zangu ni ubatili.

  4. Hakika anawatambua watu wadanganyifu; naye aonapo uovu, je, haangalii?

  5. Mpumbavu aweza kuwa mwenye hekima, endapo mtoto wa punda-mwitu atazaliwa mwanadamu.

  6. Asijidanganye mwenyewe kutumainia ubatili, kwa kuwa hatapata malipo yoyote.

  7. Mwenyezi ni nani hata tumtumikie? Tutapata faida gani kumwomba?

  8. Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na kabila za watu kula njama bure?

  9. Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu kuwa aibu mpaka lini? Mtapenda udanganyifu na kufuata miungu ya uongo mpaka lini?

  10. Kinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho; shida na ubaya viko chini ya ulimi wake.

  11. Kila mmoja humwambia jirani yake uongo; midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu.

  12. Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo.

  13. Siketi pamoja na watu wadanganyifu, wala siandamani na wanafiki,

  14. Ninawachukia wale wanaongʼangʼania sanamu batili; mimi ninamtumaini Bwana.

  15. Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya, hujitia katika njia ya dhambi na hakatai lililo baya.

  16. Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi; muda wangu wa kuishi ni kama hauna thamani kwako. Maisha ya kila mwanadamu ni kama pumzi.

  17. Hakika kila binadamu ni kama njozi aendapo huku na huko: hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili; anakusanya mali nyingi, wala hajui ni nani atakayeifaidi.

  18. Unakemea na kuadhibu wanadamu kwa ajili ya dhambi zao; unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo: kila mwanadamu ni kama pumzi tu.

  19. Kila anapokuja mtu kunitazama, huzungumza uongo, huku moyo wake hukusanya masingizio; kisha huondoka na kuyasambaza huku na huko.

  20. Tuletee msaada dhidi ya adui, kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.

  21. Binadamu wa ngazi ya chini ni pumzi tu, nao wa ngazi ya juu ni uongo tu; wakipimwa kwenye mizani, si chochote; wote kwa pamoja ni pumzi tu.

  22. Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili na miaka yao katika vitisho.

  23. Bwana anajua mawazo ya mwanadamu; anajua kwamba ni ubatili.

  24. Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.

  25. Ninachukia watu wa nia mbili, lakini ninapenda sheria yako.