Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Soldiers: Mock Jesus

13 mistari · 13 vipengele

Mistari kuhusu Mock Jesus

  1. Kisha askari wa mtawala wakampeleka Yesu kwenye Praitorio na wakakusanya kikosi kizima cha askari kumzunguka.

  2. Wakamvua nguo zake na kumvika vazi la rangi nyekundu, kisha

  3. wakasokota taji ya miiba, wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, na wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki, wakisema, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!”

  4. Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga kichwani tena na tena.

  5. Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka ili wakamsulubishe.

  6. Askari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani wa jumba la kifalme, ndio Praitorio, wakakusanya kikosi kizima cha askari.

  7. Wakamvalisha Yesu joho la zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani.

  8. Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!”

  9. Wakampiga kwa fimbo ya mwanzi tena na tena kichwani na kumtemea mate. Wakapiga magoti mbele yake, wakamsujudia kwa kumdhihaki.

  10. Walipokwisha kumdhihaki, wakamvua lile joho la zambarau, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakamtoa nje ili wakamsulubishe.

  11. Herode na askari wake wakamdhihaki Yesu na kumfanyia mzaha. Wakamvika vazi zuri sana, wakamrudisha kwa Pilato.

  12. Askari nao wakaja, wakamdhihaki. Wakamletea siki ili anywe,

  13. na wakamwambia, “Kama wewe ni Mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe.”