Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Peace

68 mistari · 38 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Hivyo Abramu akamwambia Loti, “Pasiwe na ugomvi wowote kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wako, kwa kuwa sisi ni ndugu.

  2. Je, nchi yote haiko mbele yako? Tutengane. Kama ukielekea kushoto, nitakwenda kulia; kama ukielekea kulia, mimi nitakwenda kushoto.”

  3. kwamba hutatudhuru, kama jinsi nasi hatukuwanyanyasa bali tuliwatendea mema wakati wote na kuwaondoa kwetu kwa amani. Tena sasa umebarikiwa na Bwana.’ ”

  4. Akaagana na ndugu zake walipokuwa wakiondoka, akawaambia, “Msigombane njiani!”

  5. “ ‘Nitawapa amani katika nchi, mpate kulala pasipo kutiwa hofu na yeyote. Nitawaondoa wanyama wakali watoke kwenye nchi, nao upanga hautapita katika nchi yenu.

  6. Mordekai Myahudi alikuwa wa pili kwa cheo kutoka Mfalme Ahasuero, naye alikuwa bora kabisa miongoni mwa Wayahudi, akipandishwa katika heshima ya juu na ndugu zake Wayahudi kwa sababu aliwatendea mema watu wake, na alizungumza kwa ajili ya ustawi wa Wayahudi wote.

  7. “Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi; kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi.

  8. Kwa kuwa utakuwa na agano na mawe ya mashamba, nao wanyama wa mwitu watakuwa na amani nawe.

  9. Utajua ya kwamba hema lako li salama; utahesabu mali zako wala hutakuta chochote kilichopungua.

  10. Nitamsifu Bwana ambaye hunishauri, hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha.

  11. Usiniburute pamoja na waovu, pamoja na hao watendao mabaya, ambao huzungumza na jirani zao maneno mazuri, lakini mioyoni mwao wameficha chuki.

  12. Yeyote kati yenu anayependa uzima na kutamani kuziona siku nyingi njema,

  13. Aache uovu, atende mema, aitafute amani na kuifuatilia.

  14. Hawazungumzi kwa amani, bali wanatunga mashtaka ya uongo dhidi ya wale wanaoishi kwa utulivu katika nchi.

  15. Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani.

  16. Mimi ni mtu wa amani; lakini ninaposema, wao wanataka vita.

  17. Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wakupendao na wawe salama.

  18. Amani na iwepo ndani ya kuta zako na usalama ndani ya ngome zako.”

  19. Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki, nitasema, “Amani iwe ndani yako.”

  20. Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka, Bwana atawafukuza pamoja na watenda mabaya. Amani iwe juu ya Israeli.

  21. nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.

  22. Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!

  23. Huwapa amani mipakani mwenu na kukushibisha kwa ngano safi kabisa.

  24. Upo udanganyifu katika mioyo ya wale ambao hupanga mabaya, bali kuna furaha kwa wale wanaoleta amani.

  25. Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki.