Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Ostriches

15 mistari · 3 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga, shakwe, aina zote za kipanga,

  2. mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga wa aina yoyote,

  3. Nimekuwa ndugu wa mbweha, rafiki wa mabundi.

  4. “Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa furaha, lakini hayawezi kulinganishwa na mabawa na manyoya ya korongo.

  5. Huyataga mayai yake juu ya ardhi, na kuyaacha yapate joto mchangani,

  6. bila kujali kuwa mguu waweza kuyaponda, kwamba baadhi ya wanyama wa porini wanaweza kuyakanyaga.

  7. Yeye huyafanyia makinda yake ukatili kama vile si yake; hajali kwamba taabu yake inaweza ikawa bure,

  8. kwa kuwa Mungu hakumjalia hekima, wala hakumpa fungu la akili njema.

  9. Lakini akunjuapo mabawa yake kukimbia, humcheka farasi pamoja na yeye aliyempanda.

  10. Lakini viumbe wa jangwani watalala huko, mbweha watajaza nyumba zake, bundi wataishi humo nao mbuzi-mwitu watarukaruka humo.

  11. Miiba itaenea katika ngome za ndani, viwawi na michongoma itaota kwenye ngome zake. Itakuwa maskani ya mbweha, makao ya bundi.

  12. Wanyama wa mwituni wataniheshimu, mbweha na bundi, kwa sababu ninawapatia maji jangwani, na vijito katika nchi kame, ili kuwapa watu wangu maji, wale niliowachagua,

  13. “Kwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo, nao bundi watakaa humo. Kamwe haitakaliwa tena wala watu hawataishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.

  14. Hata mbweha hutoa matiti yao kunyonyesha watoto wao, lakini watu wangu wamekuwa wasio na huruma kama mbuni jangwani.

  15. Kwa ajili ya hili nitalia na kuomboleza; nitatembea bila viatu na tena uchi. Nitabweka kama mbweha na kuomboleza kama bundi.