Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Moth

10 mistari · 3 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. ni mara ngapi zaidi wale waishio katika nyumba za udongo wa mfinyanzi, ambazo misingi yake ipo mavumbini, ambao wamepondwa kama nondo!

  2. “Hivyo mwanadamu huangamia kama kitu kilichooza, kama vazi lililoliwa na nondo.

  3. Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, kama kibanda alichotengeneza mlinzi.

  4. Unakemea na kuadhibu wanadamu kwa ajili ya dhambi zao; unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo: kila mwanadamu ni kama pumzi tu.

  5. Ni Bwana Mwenyezi anisaidiaye mimi. Ni nani huyo atakayenihukumu? Wote watachakaa kama vazi, nondo watawala wawamalize.

  6. Kwa maana nondo atawala kama vazi, nao funza atawatafuna kama sufu. Lakini haki yangu itadumu milele, wokovu wangu kwa vizazi vyote.”

  7. Mimi ni kama nondo kwa Efraimu, na kama uozo kwa watu wa Yuda.

  8. “Msijiwekee hazina duniani, mahali ambapo nondo na kutu huharibu, nao wevi huvunja na kuiba.

  9. Lakini jiwekeeni hazina mbinguni, mahali ambapo nondo na kutu haviharibu, wala wevi hawavunji na kuiba.

  10. Utajiri wenu umeoza na mavazi yenu yameliwa na nondo.