Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Missions

60 mistari · 3 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Ndipo mfalme wa Ashuru akaamuru hivi: “Mtwae mmoja wa makuhani uliowachukua mateka kutoka Samaria ili arudi kuishi humo na awafundishe watu kile ambacho Mungu wa nchi anataka.”

  2. Basi mmoja wa makuhani ambaye alikuwa amepelekwa uhamishoni kutoka Samaria akaja kuishi Betheli na kuwafundisha jinsi ya kumwabudu Bwana.

  3. Mwimbieni Bwana dunia yote; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.

  4. Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

  5. Kwa hiyo nitakusifu katikati ya mataifa, Ee Bwana; nitaliimbia sifa jina lako.

  6. Mwimbieni Bwana wimbo mpya; mwimbieni Bwana dunia yote.

  7. Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.

  8. Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

  9. Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.

  10. Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini Bwana aliziumba mbingu.

  11. Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.

  12. Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa, mpeni Bwana utukufu na nguvu.

  13. Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake.

  14. Mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake; dunia yote na itetemeke mbele zake.

  15. Katikati ya mataifa semeni, “Bwana anatawala.” Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa; atawahukumu watu kwa uadilifu.

  16. Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;

  17. mashamba na yashangilie, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha;

  18. itaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja, anakuja kuihukumu dunia. Ataihukumu dunia kwa haki, na mataifa katika kweli yake.

  19. Nitaiambia kaskazini, ‘Watoe!’ nayo kusini, ‘Usiwazuie.’ Walete wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia:

  20. kila mmoja ambaye ameitwa kwa Jina langu, niliyemuumba kwa utukufu wangu, niliyemhuluku na kumfanya.”

  21. Ndipo neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili:

  22. “Ondoka uende katika mji mkubwa wa Ninawi, ukautangazie ujumbe ninaokupa.”

  23. Yona akalitii neno la Bwana naye akaenda Ninawi. Basi Ninawi ulikuwa mji maarufu sana, ilichukua siku tatu kuuzunguka.

  24. Siku ya kwanza, Yona aliingia mjini. Akatangaza: “Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.”

  25. Watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, watu wote kuanzia mkubwa sana hadi yule mdogo kabisa, wakavaa nguo za gunia.