Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Death: Of the wicked

48 mistari · 6 vipengele

Mistari kuhusu Of the wicked

Chuja kwa kitabu
  1. “Hakika unajua jinsi ilivyokuwa tangu zamani, tangu zamani mwanadamu alipowekwa duniani,

  2. macheko ya mtu mwovu ni ya muda mfupi, nayo furaha ya wasiomcha Mungu hudumu kwa kitambo tu.

  3. “Lakini ni mara ngapi taa ya waovu huzimwa? Ni mara ngapi maafa huwajia, yale yawapatayo ambayo Mungu huwapangia katika hasira yake?

  4. Ni mara ngapi huwa kama majani makavu mbele ya upepo, kama makapi yachukuliwayo na dhoruba?

  5. Mtu mmoja hufa akiwa na nguvu zake kamili, akiwa salama na mwenye raha kamili,

  6. mwili wake ukiwa umenawiri, nayo mifupa yake ikiwa imejaa mafuta ndani yake.

  7. Mtu mwingine hufa katika uchungu wa nafsi, akiwa hajafurahia kamwe jambo lolote zuri.

  8. Hao wote hulala mavumbini, nao mabuu huwafunika wote.

  9. Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; afunguapo macho yake, yote yametoweka.

  10. Vitisho humjia kama mafuriko; dhoruba humkumba ghafula usiku.

  11. Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; humzoa kutoka mahali pake.

  12. Humvurumisha bila huruma, huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake.

  13. Upepo humpigia makofi kwa dharau, na kumfukuza atoke mahali pake.

  14. Zaburi ya Daudi. Usisumbuke kwa ajili ya watendao maovu, wala usiwaonee wivu watendao mabaya,

  15. kwa maana kama majani watanyauka mara, kama mimea ya kijani watakufa mara.

  16. Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi.

  17. Bado kitambo kidogo, nao waovu hawataonekana, ingawa utawatafuta, hawataonekana.

  18. Nimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi kama mwerezi wa Lebanoni,

  19. lakini alitoweka mara na hakuonekana, ingawa nilimtafuta, hakupatikana.

  20. ili kwamba aishi milele na asione uharibifu.

  21. Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali zao.

  22. atajiunga na kizazi cha baba zake, ambao hawataona kamwe nuru ya uzima.

  23. Mwanadamu mwenye utajiri bila ufahamu ni kama wanyama waangamiao.

  24. Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna nilipoona kufanikiwa kwa waovu.

  25. Wao hawana taabu, miili yao ina afya na nguvu.