Rukia maudhui

Aaron

331 mistari · 9 wanafamilia

Mistari inayomtaja Aaron

Chuja kwa kitabu
  1. Kisha Daudi akawakusanya pamoja wazao wa Aroni na Walawi:

  2. Wana wa Amramu walikuwa: Aroni na Mose. Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za Bwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la Bwana milele.

  3. Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aroni kuhudumu katika Hekalu la Bwana: Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wowote katika nyumba ya Mungu.

  4. Hivyo Walawi wakafanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, katika Mahali Patakatifu chini ya uongozi wa ndugu zao wazao wa Aroni, kwa ajili ya utumishi katika Hekalu la Bwana.

  5. Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni: Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

  6. Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Bwana kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.

  7. Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.

  8. Lakini je, hamkuwafukuza makuhani wa Bwana, wana wa Aroni na Walawi na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama yafanyavyo mataifa ya nchi nyingine? Yeyote anayekuja kujiweka wakfu akiwa na ndama dume na kondoo dume saba aweza kuwa kuhani wa kile ambacho ni miungu kwenu.

  9. “Lakini kwetu sisi, Bwana ndiye Mungu wetu, wala hatujamwacha. Makuhani wanaomtumikia Bwana ni wana wa Aroni, nao Walawi wakiwasaidia.

  10. Wakamkabili na kumwambia, “Siyo sawa kwako, Uzia, kumfukizia Bwana uvumba. Hiyo ni kazi ya makuhani, wazao wa Aroni, ambao wamewekwa wakfu ili kufukiza uvumba. Ondoka mahali patakatifu, kwa kuwa umekosa uaminifu nawe hutaheshimiwa na Bwana.”

  11. Wakaleta mafahali saba, kondoo dume saba, wana-kondoo dume saba na mabeberu saba kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya ufalme, kwa ajili ya mahali patakatifu na kwa ajili ya Yuda. Mfalme akawaamuru makuhani, wazao wa Aroni, kuvitoa vitu hivyo sadaka katika madhabahu ya Bwana.

  12. Kuhusu makuhani, wazao wa Aroni walioishi kwenye mashamba yaliyozunguka miji yao au katika miji mingine yoyote, watu walitajwa majina ili kumgawia kila mwanaume miongoni mwao na kwa wote waliokuwa katika orodha ya vizazi vya Walawi.

  13. Hatimaye wakafanya maandalizi kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, kwa sababu wale makuhani, yaani, wazao wa Aroni, walikuwa wanatoa sadaka za kuteketezwa pamoja na zile sehemu zilizonona mpaka usiku. Hivyo Walawi wakafanya maandalizi kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani wa uzao wa Aroni.

  14. mwana wa Abishua, mwana wa Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani mkuu Aroni.

  15. Kuhani atokanaye na uzao wa Aroni atashirikiana na Walawi wakati wanapopokea zaka, nao Walawi itawapasa kuleta sehemu ya kumi ya zaka katika nyumba ya Mungu wetu katika ghala za hazina.

  16. Kwa hiyo katika siku za Zerubabeli na za Nehemia, Israeli wote walitoa mafungu kila siku kwa ajili ya waimbaji na mabawabu. Pia walitenga fungu kwa ajili ya Walawi wengine, nao Walawi walitenga fungu kwa ajili ya wazao wa Aroni.

  17. Uliongoza watu wako kama kundi kwa mkono wa Mose na Aroni.

  18. Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita Bwana, naye aliwajibu.

  19. Akamtuma Mose mtumishi wake, pamoja na Aroni, aliyemchagua.

  20. Kambini walimwonea wivu Mose, na pia Aroni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Bwana.

  21. Ee nyumba ya Aroni, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao.

  22. Bwana anatukumbuka na atatubariki: ataibariki nyumba ya Israeli, ataibariki nyumba ya Aroni,

  23. Nyumba ya Aroni na iseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”

  24. Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, yakitiririka kwenye ndevu, yakitiririka kwenye ndevu za Aroni, mpaka kwenye upindo wa mavazi yake.

  25. Ee nyumba ya Israeli, msifuni Bwana; ee nyumba ya Aroni, msifuni Bwana;