Zaburi 44:9-22
9
Lakini sasa umetukataa na kutudhili, wala huendi tena na jeshi letu.
10
Umetufanya turudi nyuma mbele ya adui, nao watesi wetu wametuteka nyara.
11
Umetuacha tutafunwe kama kondoo na umetutawanya katika mataifa.
12
Umewauza watu wako kwa fedha kidogo, wala hukupata faida yoyote kwa mauzo yao.
13
Umetufanya lawama kwa jirani zetu, dharau na dhihaka kwa wale wanaotuzunguka.
14
Umetufanya kuwa mithali miongoni mwa mataifa, mataifa hutikisa vichwa vyao.
15
Fedheha yangu iko mbele yangu mchana kutwa, na uso wangu umejaa aibu tele,
16
kwa ajili ya dhihaka ya wale wanaonilaumu na kunitukana, kwa sababu ya adui, ambaye anatamani kulipiza kisasi.
17
Hayo yote yametutokea, ingawa tulikuwa hatujakusahau wala hatujaenda kinyume na agano lako.
18
Mioyo yetu ilikuwa haijarudi nyuma; nyayo zetu zilikuwa hazijaiacha njia yako.
19
Lakini ulituponda na kutufanya makao ya mbweha, na ukatufunika kwa giza nene.
20
Kama tungalikuwa tumelisahau jina la Mungu wetu au kunyooshea mikono yetu kwa mungu mgeni,
21
je, Mungu hangaligundua hili, kwa kuwa anazijua siri za moyo?
22
Hata hivyo kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa; tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.
Settings