Rukia maudhui
Zaburi 17:1-7

Zaburi 17:1-7

1
Sala ya Daudi. Sikia, Ee Bwana, kusihi kwangu kwa haki, sikiliza kilio changu. Tega sikio kwa ombi langu, halitoki kwenye midomo ya udanganyifu.
2
Hukumu yangu na itoke kwako, macho yako na yaone yale yaliyo haki.
3
Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku, ingawa umenijaribu, hutaona chochote. Nimeamua kwamba kinywa changu hakitatenda dhambi.
4
Kuhusu matendo ya wanadamu: kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za wenye jeuri.
5
Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; nyayo zangu hazikuteleza.
6
Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, nitegee sikio lako na usikie ombi langu.
7
Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options