Skip to content
Yohana 16:1-18

Yohana 16:1-18

1
“Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkaiacha imani.
2
Watawatenga na masinagogi. Naam, saa yaja ambayo mtu yeyote atakayewaua atadhani kwa kufanya hivyo anamtumikia Mungu.
3
Nao watawatenda haya kwa sababu hawamjui Baba wala mimi.
4
Lakini nimewaambia ninyi mambo haya, ili saa hiyo ikiwadia mpate kukumbuka ya kuwa nilikuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.
5
“Sasa mimi ninakwenda kwake yeye aliyenituma, lakini hakuna hata aniulizaye, ‘Unakwenda wapi?’
6
Kwa sababu nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni.
7
Lakini nawaambia kweli, yafaa mimi niondoke, kwa kuwa nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu, lakini nikienda nitamtuma kwenu.
8
Naye atakapokuja, atauthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi, haki na hukumu.
9
Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi,
10
kwa habari ya haki, kwa sababu ninakwenda kwa Baba, nanyi hamtaniona tena,
11
kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.
12
“Bado ninayo mambo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili sasa.
13
Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonyesha mambo yajayo.
14
Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi.
15
Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu. Ndiyo maana nimesema Roho atachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi.
16
“Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona.”
17
Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona’? Naye ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninakwenda kwa Baba’?”
18
Wakaendelea kuulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Kitambo kidogo’? Hatuelewi hilo analosema.”
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options