- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
Ayubu12
Listen to this chapter
0:00
0:00
Ayubu awakaripia rafiki zake kwa kiburi
1
Ndipo Ayubu akajibu:
2
“Bila shaka ninyi ndio watu, nayo hekima itakoma mtakapokufa!
3
Lakini mimi ninao ufahamu kama ninyi; mimi si duni kwenu. Ni nani asiyejua mambo haya yote?
4
“Nimekuwa mtu wa kuchekwa na rafiki zangu, ingawa nilimwita Mungu naye akanijibu: mimi ni mtu wa kuchekwa tu, ingawa ni mwadilifu na nisiye na hatia!
5
Wanadamu wakiwa katika utulivu huwa na dharau kwa wale wenye msiba kana kwamba ndiyo haki ya wale ambao miguu yao inateleza.
6
Hema za wanyangʼanyi hazisumbuliwi, wale wanaomghadhibisha Mungu wako salama: wale wamchukuao mungu wao mikononi mwao.
Asili yashuhudia utawala wa Mungu
7
“Lakini ulizeni wanyama, nao watawafundisha, au ndege wa angani, nao watawaambia;
8
au zungumzeni na dunia, nayo itawafundisha, au acheni samaki wa baharini wawape taarifa.
9
Ni nani miongoni mwa hawa wote asiyejua kwamba mkono wa Bwana ndio uliofanya hili?
10
Mkononi mwake kuna uhai wa kila kiumbe, na pumzi ya wanadamu wote.
11
Je, sikio haliyajaribu maneno kama vile ulimi uonjavyo chakula?
12
Je, hekima haipatikani katikati ya wazee? Je, maisha marefu hayaleti ufahamu?
Enzi kuu ya Mungu isiyodhibitika
13
“Hekima na nguvu ni vya Mungu; shauri na ufahamu ni vyake yeye.
14
Kile anachokibomoa hakiwezi kujengeka tena; mtu aliyefungiwa naye hawezi kufunguliwa.
15
Akizuia maji, huwa pana ukame; akiyaachia maji, huharibu nchi.
16
Kwake kuna nguvu na ushindi; adanganywaye na adanganyaye, wote wawili ni wake.
17
Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara, naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi.
18
Huondoa pingu zilizofungwa na wafalme, na kuwafunga mishipi ya kiunoni.
19
Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu.
20
Hunyamazisha midomo ya washauri wanaoaminika, na kuondoa busara ya wazee.
21
Huwamwagia dharau wanaoheshimika, na kuwavua silaha wenye nguvu.
22
Hufunua mambo ya ndani ya gizani, na kuyaleta nuruni yale yaliyositirika sana.
23
Huyafanya mataifa yatukuke na kuyaangamiza; hufanya mataifa kuwa makubwa, naye huyatawanya.
24
Huwaondolea viongozi wa nchi akili zao; huwapeleka watangetange nyikani pasipo na njia.
25
Hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga; huwafanya wapepesuke kama walevi.
Use ← → arrow keys to navigate
Settings
Reading Style
Typeface
Font Size px
Reading Width chars
Options
Study Note