Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Poor: Unclassified scriptures relating to

72 mistari · 4 vipengele

Mistari kuhusu Unclassified scriptures relating to

Chuja kwa kitabu
  1. nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake.

  2. “Usiwanyime haki watu wako walio maskini katika mashtaka yao.

  3. “ ‘Usipotoshe haki; usionyeshe kumpendelea maskini, wala upendeleo kwa mwenye cheo, bali mwamulie jirani yako kwa haki.

  4. Bwana humfanya mtu maskini naye hutajirisha, hushusha na hukweza.

  5. Nehemia akasema, “Nendeni mkafurahie chakula kizuri na vinywaji vitamu, na mpeleke sehemu kwa wale ambao hawana chochote cha kula. Siku hii ni takatifu kwa Bwana. Msihuzunike, kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.”

  6. Kisha watu wote wakaondoka kwenda kula na kunywa, na kupeana sehemu ya chakula, na wakaadhimisha kwa furaha kubwa, kwa sababu sasa walifahamu maneno yale waliyokuwa wameelezwa.

  7. Yeyote aliyenisikia alinena mema juu yangu, nao walioniona walinisifu,

  8. kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada, naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia.

  9. Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki, nami niliufanya moyo wa mjane kuimba.

  10. Nilikuwa macho ya kipofu na miguu kwa kiwete.

  11. Nilikuwa baba kwa mhitaji; nilimtetea mgeni.

  12. Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu? Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini?

  13. Je, yeye aliyeniumba tumboni mwa mama yangu, si ndiye aliwaumba? Je, si ni yeye huyo mmoja aliyetuumba sote ndani ya mama zetu?

  14. “Ikiwa nimewanyima maskini haja zao, au kuyaacha macho ya wajane yadhoofike,

  15. kama nimekula chakula changu mwenyewe, bila kuwashirikisha yatima;

  16. lakini tangu ujana wangu nimemlea yatima kama ambavyo baba angefanya, nami tangu kuzaliwa kwangu nimewaongoza wajane:

  17. kama nilimwona yeyote akiteseka kwa kukosa nguo, au mtu mhitaji asiye na mavazi

  18. ambaye wala moyo wake haukunibariki kwa kumpatia joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo zangu,

  19. na kama nimeinua mkono wangu dhidi ya yatima, nikijua kuwa nina ushawishi mahakamani,

  20. basi mkono wangu na unyofoke toka begani mwangu, nao na uvunjike kutoka kiungio chake.

  21. yeye asiyependelea wakuu, wala haonyeshi upendeleo kwa matajiri kuliko maskini, kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake?

  22. Bora kidogo walicho nacho wenye haki kuliko wingi wa mali wa waovu wengi;

  23. Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na walioonewa.

  24. Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.

  25. Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema, bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo.