Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Perfection

71 mistari · 19 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Abramu alipokuwa na miaka tisini na tisa, Bwana akamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi; enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu.

  2. Hivyo kuweni waangalifu kuyafanya yale Bwana Mungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto.

  3. Kamwe msilaumiwe mbele za Bwana Mungu wenu.

  4. “Kuweni hodari sana, kuweni waangalifu kutii yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Sheria ya Mose, pasipo kugeuka upande wa kuume au kushoto.

  5. Lakini ni lazima mwiweke mioyo yenu kikamilifu kwa Bwana Mungu wetu, kuishi kwa maagizo yake na kutii amri zake, kama ilivyo wakati huu.”

  6. “Nawe Solomoni mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maana Bwana huuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako; bali kama ukimwacha, yeye atakukataa milele.

  7. Nawe umpe mwanangu Solomoni kujitolea kwako kwa moyo wote ili kuzishika amri zako, masharti yako, maagizo yako na kufanya kila kitu ili kujenga Hekalu hili la fahari ambalo kwa ajili yake nimetoa.”

  8. “Watakapotenda dhambi dhidi yako, kwa kuwa hakuna mtu yeyote ambaye hatendi dhambi, nawe ukachukizwa nao na kuwakabidhi kwa adui, ambaye atawachukua utumwani katika nchi iliyo mbali au karibu

  9. Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu; kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia.

  10. “Ingawa mimi sina kosa, haileti tofauti katika nafsi yangu; nauchukia uhai wangu.

  11. Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.

  12. Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake; nyayo zake hazitelezi.

  13. Watafakari watu wasio na hatia, wachunguze watu wakamilifu, kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani.

  14. Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama: utakuja kwangu lini? Nitatembea nyumbani mwangu kwa moyo usio na lawama.

  15. Heri wale wanaodumisha haki, ambao daima wanafanya yaliyo mema.

  16. Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika sheria ya Bwana.

  17. Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wao wote.

  18. Wasiofanya lolote lililo baya, wanaoenenda katika njia zake.

  19. Hivyo mimi sitaaibishwa ninapozingatia amri zako zote.

  20. Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo, lakini amri zako hazina mpaka.

  21. Bwana atatimiza kusudi lake kwangu, Ee Bwana, upendo wako wadumu milele: usiziache kazi za mikono yako.

  22. Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi, nao wasio na lawama watabakia ndani yake.

  23. Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko, ambayo hungʼaa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu.

  24. Hakuna mtu mwenye haki duniani ambaye hufanya mambo ya haki na kamwe asitende dhambi.

  25. Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watatoshelezwa.