Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Meditation

42 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Isaki akatoka kwenda shambani kutafakari wakati wa jioni, alipoinua macho yake, akaona ngamia wanakuja.

  2. Usiache Kitabu hiki cha Sheria kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi.

  3. Bali huifurahia sheria ya Bwana, naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana.

  4. Katika hasira yako, usitende dhambi. Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya mkiichunguza mioyo yenu.

  5. Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu na Mkombozi wangu.

  6. Moyo wangu ulipata moto ndani yangu, nilipotafakari, moto uliwaka, ndipo nikasema kwa ulimi wangu:

  7. Kinywa changu kitasema maneno ya hekima, usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu.

  8. Nafsi yangu itatoshelezwa kama kwa wingi wa vyakula; kwa midomo iimbayo kinywa changu kitakusifu wewe.

  9. Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe, ninawaza juu yako makesha yote ya usiku.

  10. Hivi ndivyo walivyo waovu: siku zote hawajali, wanaongezeka katika utajiri.

  11. Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure, ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia.

  12. Mchana kutwa nimetaabika, nimeadhibiwa kila asubuhi.

  13. Kama ningesema, “Nitasema hivi,” ningelikuwa nimewasaliti watoto wako.

  14. Nilipojaribu kuelewa haya yote, yalikuwa magumu kwangu kuelewa.

  15. Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu, ndipo nilipotambua mwisho wao.

  16. Hakika unawaweka mahali pa utelezi, unawaangusha chini kwa uharibifu.

  17. Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula, wanatoweshwa kabisa na vitisho!

  18. Kama ndoto mtu aamkapo, hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana, utawatowesha kama ndoto.

  19. Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa, na roho yangu ilipotiwa uchungu,

  20. nilikuwa mpumbavu na mjinga, nilikuwa mnyama mkatili mbele yako.

  21. Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu: lakini nitakumbuka miaka ya mkono wa kuume wa Aliye Juu Sana.”

  22. Nitayakumbuka matendo ya Bwana; naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani.

  23. Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu.

  24. Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye, ninapofurahi katika Bwana.

  25. Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.