Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Man

106 mistari · 114 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kwa hiyo siku zote tunalo tumaini, hata ingawa tunajua kwamba wakati tukiwa katika mwili huu, tuko mbali na Bwana,

  2. kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona.

  3. Naam, tunalo tumaini na ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili huu na kwenda kukaa na Bwana.

  4. Kwa hiyo, kama tuko katika mwili huu au tuko mbali nao, lengo letu ni kumpendeza Bwana.

  5. Umemfanya chini kidogo kuliko malaika; ukamvika taji ya utukufu na heshima,

  6. nawe umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Kwa kuweka vitu vyote chini yake, Mungu hakuacha kitu chochote ambacho hakukiweka chini ya mwanadamu. Lakini kwa sasa, hatuoni kwamba kila kitu kiko chini yake.