Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Heart: Unclassified scriptures descriptive of the seat of the affections

13 mistari · 2 vipengele

Mistari kuhusu Unclassified scriptures descriptive of the seat of the affections

  1. Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

  2. Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako.

  3. Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke, bali maumivu ya moyoni huponda roho.

  4. Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hujilisha upumbavu.

  5. Siku zote za wanaoonewa ni za taabu, bali moyo mchangamfu una karamu ya kudumu.

  6. Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, ni mwovu kupita kiasi. Ni nani awezaye kuujua?

  7. “Mimi Bwana huchunguza moyo na kuzijaribu nia, ili kumlipa mtu kwa kadiri ya mwenendo wake, kwa kadiri ya matendo yake yanavyostahili.”

  8. Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi.

  9. Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio.

  10. Haya ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula bila kunawa mikono hakumtii mtu unajisi.”

  11. (Naam, wakati wa watu wa Mataifa, ambao hawana sheria, wanapofanya kwa asili mambo yatakiwayo na sheria, wao ni sheria kwa nafsi zao wenyewe, hata ingawa hawana sheria.

  12. Wao wanaonyesha kwamba lile linalotakiwa na sheria limeandikwa kwenye mioyo yao, ambayo pia dhamiri zao zikiwashuhudia, nayo mawazo yao yenye kupingana yatawashtaki au kuwatetea.)

  13. Hili litatukia siku hiyo Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu kwa njia ya Yesu Kristo, kama isemavyo Injili yangu.