Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Anger: General references

13 mistari · 38 vipengele

Mistari kuhusu General references

  1. Hekima ya mtu humpa uvumilivu, ni kwa utukufu wake kusamehe makosa.

  2. Ghadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba, bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi.

  3. Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira ya haraka, usishirikiane na yule aliye mwepesi kukasirika,

  4. la sivyo utajifunza njia zake na kujiingiza mwenyewe kwenye mtego.

  5. Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo, lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito kuliko vyote viwili.

  6. Hasira ni ukatili na ghadhabu kali ni gharika, lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu?

  7. Wenye mzaha huuchochea mji, bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira.

  8. Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani.

  9. Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi,

  10. kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

  11. husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi Ufalme wa Mungu.

  12. Ndugu zangu wapendwa, fahamuni jambo hili: Kila mtu awe mwepesi wa kusikiliza, lakini asiwe mwepesi wa kusema wala wa kukasirika.

  13. Kwa maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu.