Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Adah

8 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Lameki alioa wanawake wawili, mmoja aliitwa Ada, na mwingine Sila.

  2. Ada akamzaa Yabali ambaye ni baba wa wale walioishi katika mahema na kufuga wanyama.

  3. Kaka yake aliitwa Yubali, aliyekuwa baba wa wote wapigao zeze na filimbi.

  4. Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini.

  5. Lameki akawaambia wake zake, “Ada na Sila nisikilizeni mimi; wake wa Lameki sikieni maneno yangu. Nimemuua mtu kwa kunijeruhi, kijana mdogo kwa kuniumiza.

  6. Haya ndiyo majina ya wana wa Esau: Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia.

  7. Wana wa Elifazi ni: Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi.

  8. Elifazi mwana wa Esau alikuwa pia na suria aliyeitwa Timna, ambaye alimzalia Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Ada mke wa Esau.