Rukia maudhui

circa 800–400 BC

The Hebrew Prophets

God speaks through Isaiah, Jeremiah, and the minor prophets—calling Israel to repentance and foretelling the coming Messiah.

3,706 mistari · 14 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Yeremia 50:14takriban 595 KK

    “Shikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli, enyi nyote mvutao upinde. Mpigeni! Msibakize mshale wowote, kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya Bwana.

  2. Yeremia 50:15takriban 595 KK

    Piga kelele dhidi yake kila upande! Anajisalimisha, minara yake inaanguka, kuta zake zimebomoka. Kwa kuwa hiki ni kisasi cha Bwana, mlipizeni kisasi; mtendeeni kama alivyowatendea wengine.

  3. Yeremia 50:16takriban 595 KK

    Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli, pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna. Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe, kila mmoja na akimbilie kwenye nchi yake mwenyewe.

  4. Yeremia 50:17takriban 595 KK

    “Israeli ni kundi lililotawanyika ambalo simba wamelifukuzia mbali. Wa kwanza kumla alikuwa mfalme wa Ashuru, wa mwisho kuponda mifupa yake alikuwa Nebukadneza mfalme wa Babeli.”

  5. Yeremia 50:18takriban 595 KK

    Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Nitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yake kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.

  6. Yeremia 50:19takriban 595 KK

    Lakini nitamrudisha Israeli katika malisho yake mwenyewe naye atalisha huko Karmeli na Bashani; njaa yake itashibishwa juu ya vilima vya Efraimu na Gileadi.

  7. Yeremia 50:20takriban 595 KK

    Katika siku hizo, wakati huo,” asema Bwana, “uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli, lakini halitakuwepo, kwa ajili ya dhambi za Yuda, lakini haitapatikana hata moja, kwa kuwa nitawasamehe mabaki nitakaowaacha.

  8. Yeremia 50:21takriban 595 KK

    “Shambulieni nchi ya Merathaimu na wale waishio huko Pekodi. Wafuatieni, waueni na kuwaangamiza kabisa,” asema Bwana. “Fanyeni kila kitu nilichowaamuru.

  9. Yeremia 50:22takriban 595 KK

    Kelele ya vita iko ndani ya nchi, kelele ya maangamizi makuu!

  10. Yeremia 50:23takriban 595 KK

    Tazama jinsi nyundo ya dunia yote ilivyovunjika na kuharibika! Tazama jinsi Babeli ilivyokuwa ukiwa miongoni mwa mataifa!

  11. Yeremia 50:24takriban 595 KK

    Nimetega mtego kwa ajili yako, ee Babeli, nawe ukakamatwa kabla haujafahamu; ulipatikana na ukakamatwa kwa sababu ulimpinga Bwana.

  12. Yeremia 50:25takriban 595 KK

    Bwana amefungua ghala lake la silaha na kuzitoa silaha za ghadhabu yake, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mwenye Nguvu Zote anayo kazi ya kufanya katika nchi ya Wakaldayo.

  13. Yeremia 50:26takriban 595 KK

    Njooni dhidi yake kutoka mbali. Zifungueni ghala zake za nafaka; mlundikeni kama lundo la nafaka. Mwangamizeni kabisa na msimwachie mabaki yoyote.

  14. Yeremia 50:27takriban 595 KK

    Waueni mafahali wake wachanga wote; waacheni washuke machinjoni! Ole wao! Kwa kuwa siku yao imewadia, wakati wao wa kuadhibiwa.

  15. Yeremia 50:28takriban 595 KK

    Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeli wakitangaza katika Sayuni jinsi Bwana, Mungu wetu alivyolipiza kisasi, kisasi kwa ajili ya Hekalu lake.

  16. Yeremia 50:29takriban 595 KK

    “Waiteni wapiga mishale dhidi ya Babeli, wote wale wavutao upinde. Pigeni kambi kumzunguka kabisa, asitoroke mtu yeyote. Mlipizeni kwa matendo yake; mtendeeni kama alivyotenda. Kwa kuwa alimdharau Bwana, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

  17. Yeremia 50:30takriban 595 KK

    Kwa hiyo, vijana wake wanaume wataanguka barabarani; askari wake wote watanyamazishwa siku ile,” asema Bwana.

  18. Yeremia 50:31takriban 595 KK

    “Tazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,” asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, “kwa kuwa siku yako imewadia, yaani, wakati wako wa kuadhibiwa.

  19. Yeremia 50:32takriban 595 KK

    Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka, wala hakuna yeyote atakayemuinua; nitawasha moto katika miji yake, utakaowateketeza wote wanaomzunguka.”

  20. Yeremia 50:33takriban 595 KK

    Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Watu wa Israeli wameonewa, nao watu wa Yuda pia. Wote waliowateka wamewashikilia sana, wanakataa kuwaachia waende.

  21. Yeremia 50:34takriban 595 KK

    Lakini Mkombozi wao ana nguvu; Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. Atatetea kwa nguvu shauri lao ili alete raha katika nchi yao, lakini ataleta msukosuko kwa wale waishio Babeli.

  22. Yeremia 50:35takriban 595 KK

    “Upanga dhidi ya Wakaldayo!” asema Bwana, “dhidi ya wale waishio Babeli na dhidi ya maafisa wake na watu wenye busara!

  23. Yeremia 50:36takriban 595 KK

    Upanga dhidi ya manabii wake wa uongo! Watakuwa wapumbavu. Upanga dhidi ya mashujaa wake! Watajazwa na hofu kuu

  24. Yeremia 50:37takriban 595 KK

    Upanga dhidi ya farasi na magari yake ya vita pamoja na askari wake wote wa kigeni katika safu zake! Wao watakuwa kama wanawake. Upanga dhidi ya hazina zake! Hizo zitatekwa nyara.

  25. Yeremia 50:38takriban 595 KK

    Ukame juu ya maji yake! Nayo yatakauka. Kwa kuwa ni nchi ya sanamu, wao wanaenda wazimu kwa ajili ya sanamu.