Rukia maudhui

circa 605–538 BC

The Babylonian Exile

Jerusalem falls and the temple burns; Ezekiel and Daniel minister among the exiles as Lamentations mourns the city's ruin.

1,784 mistari · 3 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Ezekieli 17:11takriban 594 KK

    Ndipo neno la Bwana likanijia kusema:

  2. Ezekieli 17:12takriban 594 KK

    “Waambie nyumba hii ya kuasi, ‘Je, mnajua hii ina maana gani?’ Waambie: ‘Mfalme wa Babeli alikwenda Yerusalemu na kumchukua mfalme na watu maarufu, akarudi nao na kuwaleta mpaka Babeli.

  3. Ezekieli 17:13takriban 594 KK

    Ndipo akamchukua mmoja wa jamaa ya mfalme na kufanya mapatano naye, akamfanya aape. Akawachukua pia viongozi wa nchi,

  4. Ezekieli 17:14takriban 594 KK

    ili kuudhoofisha ufalme huo, usiweze kuinuka tena, ila uweze kuendelea tu chini ya mapatano yake.

  5. Ezekieli 17:15takriban 594 KK

    Lakini mfalme aliasi dhidi yake kwa kutuma wajumbe wake kwenda Misri ili kupatiwa farasi na jeshi kubwa. Je, atashinda? Je, atafanikiwa? Je, mtu afanyaye mambo kama hayo ataokoka? Je, atavunja mapatano na bado aokoke?

  6. Ezekieli 17:16takriban 594 KK

    “ ‘Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, atafia huko Babeli, katika nchi ya mfalme aliyemketisha katika kiti cha enzi, ambaye alidharau kiapo chake na kuvunja mapatano yake.

  7. Ezekieli 17:17takriban 594 KK

    Farao na jeshi lake kubwa, na wingi wake wa watu hawataweza kusaidia chochote katika vita, wakati watakapozungukwa na jeshi ili kukatilia mbali maisha ya watu wengi.

  8. Ezekieli 17:18takriban 594 KK

    Alidharau kiapo kwa kuvunja Agano. Kwa sababu aliahidi kwa mkono wake mwenyewe na bado akafanya mambo haya yote, hataokoka.

  9. Ezekieli 17:19takriban 594 KK

    “ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, nitaleta juu ya kichwa chake kiapo changu, alichokidharau na Agano langu lile alilolivunja.

  10. Ezekieli 17:20takriban 594 KK

    Nitautandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa katika mtego wangu. Nitamleta mpaka Babeli na kutekeleza hukumu juu yake huko kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwangu.

  11. Ezekieli 17:21takriban 594 KK

    Askari wake wote wanaotoroka wataanguka kwa upanga, nao watakaonusurika watatawanyika katika pande zote za dunia. Ndipo utakapojua kuwa Mimi Bwana nimesema.

  12. Ezekieli 17:22takriban 594 KK

    “ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitachukua chipukizi kutoka kwenye kilele cha juu sana cha mwerezi na kukipanda, nitavunja kitawi kichanga kutoka matawi yake ya juu kabisa na kukipanda juu ya mlima mrefu ulioinuka sana.

  13. Ezekieli 17:23takriban 594 KK

    Katika vilele vya mlima mrefu wa Israeli nitakipanda, kitatoa matawi na kuzaa matunda na kuwa mwerezi mzuri sana. Ndege wa kila aina wataweka viota vyao ndani yake, nao watapata makazi katika kivuli cha matawi yake.

  14. Ezekieli 17:24takriban 594 KK

    Miti yote ya kondeni itajua kuwa Mimi Bwana ninaishusha miti mirefu na kuikuza miti mifupi kuwa miti mirefu. Mimi naikausha miti mibichi na kuifanya miti mikavu istawi. “ ‘Mimi Bwana nimesema, nami nitatenda.’ ”

  15. Ezekieli 18:1takriban 594 KK

    Neno la Bwana likanijia kusema:

  16. Ezekieli 18:2takriban 594 KK

    “Je, ninyi watu mna maana gani kutumia mithali hii inayohusu nchi ya Israeli: “ ‘Baba wamekula zabibu zenye chachu, nayo meno ya watoto yametiwa ganzi’?

  17. Ezekieli 18:3takriban 594 KK

    “Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hamtatumia tena mithali hii katika Israeli.

  18. Ezekieli 18:4takriban 594 KK

    Kwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa.

  19. Ezekieli 18:5takriban 594 KK

    “Mtu aweza kuwa ni mwenye haki atendaye yaliyo haki na sawa.

  20. Ezekieli 18:6takriban 594 KK

    Hakula katika mahali pa ibada za miungu kwenye milima wala hakuziinulia macho sanamu za nyumba ya Israeli. Hakumtia unajisi mke wa jirani yake, wala hakukutana kimwili na mwanamke wakati wa siku zake za hedhi.

  21. Ezekieli 18:7takriban 594 KK

    Hamwonei mtu yeyote, bali hurudisha kilichowekwa rehani kwake. Hanyangʼanyi, bali huwapa wenye njaa chakula chake na huwapa nguo walio uchi.

  22. Ezekieli 18:8takriban 594 KK

    Hakopeshi kwa riba wala hajipatii faida ya ziada. Huuzuia mkono wake usifanye mabaya, naye huhukumu kwa haki kati ya mtu na mtu.

  23. Ezekieli 18:9takriban 594 KK

    Huzifuata amri zangu na kuzishika sheria zangu kwa uaminifu. Huyo mtu ni mwenye haki; hakika ataishi, asema Bwana Mwenyezi.

  24. Ezekieli 18:10takriban 594 KK

    “Aweza kuwa ana mwana jeuri, amwagaye damu au atendaye mojawapo ya mambo haya

  25. Ezekieli 18:11takriban 594 KK

    (ingawa baba yake hakufanya mojawapo ya haya): “Hula katika mahali pa ibada za miungu kwenye milima. Humtia unajisi mke wa jirani yake.