Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Walawi 19:17takriban 1490 KK

    “ ‘Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Karipia jirani yako kwa uwazi ili usishiriki hatia yake.

  2. Walawi 19:18takriban 1490 KK

    “ ‘Usijilipizie kisasi wala kuwa na kinyongo dhidi ya mmoja wa jamaa yako, lakini mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Bwana.

  3. Walawi 19:19takriban 1490 KK

    “ ‘Mtazishika amri zangu. “ ‘Usiwaache wanyama wako wa kufugwa wakazaana na wengine wa aina tofauti. “ ‘Usipande mbegu za aina mbili katika shamba lako. “ ‘Usivae nguo iliyofumwa kwa nyuzi za aina mbili tofauti.

  4. Walawi 19:20takriban 1490 KK

    “ ‘Kama mwanaume anakutana kimwili na mwanamke ambaye ni msichana mtumwa aliyeposwa na mwanaume mwingine, lakini ambaye hajakombolewa wala hajapewa uhuru, lazima iwepo adhabu inayofaa. Hata hivyo hawatauawa, kwa sababu msichana alikuwa bado hajaachwa huru.

  5. Walawi 19:21takriban 1490 KK

    Lakini huyo mtu lazima alete kondoo dume kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa ajili ya sadaka ya hatia kwa Bwana.

  6. Walawi 19:22takriban 1490 KK

    Kupitia kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana kwa ajili ya dhambi aliyotenda, naye atasamehewa dhambi yake.

  7. Walawi 19:23takriban 1490 KK

    “ ‘Mtakapoingia katika hiyo nchi na kupanda aina yoyote ya mti wa matunda, hesabuni matunda yake kama yaliyokatazwa. Kwa miaka mitatu mtayahesabu kwamba yamekatazwa; hayaruhusiwi kuliwa.

  8. Walawi 19:24takriban 1490 KK

    Katika mwaka wa nne matunda yote ya mti huo yatakuwa matakatifu, sadaka ya sifa kwa Bwana.

  9. Walawi 19:25takriban 1490 KK

    Bali katika mwaka wa tano mnaweza kula matunda ya mti huo. Kwa njia hii mavuno yenu yataongezewa. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

  10. Walawi 19:26takriban 1490 KK

    “ ‘Msile nyama yoyote yenye damu ndani yake. “ ‘Msifanye uaguzi wala uchawi.

  11. Walawi 19:27takriban 1490 KK

    “ ‘Msikate nywele za kichwa denge, wala kunyoa pembe za ndevu zenu.

  12. Walawi 19:28takriban 1490 KK

    “ ‘Msichanje chale miili yenu kwa ajili ya mfu, wala msijichore alama juu ya miili yenu. Mimi ndimi Bwana.

  13. Walawi 19:29takriban 1490 KK

    “ ‘Usimdhalilishe binti yako kwa kumfanya kahaba, la sivyo nchi itageukia ukahaba na kujaa uovu.

  14. Walawi 19:30takriban 1490 KK

    “ ‘Shika Sabato zangu na kuheshimu mahali pangu patakatifu. Mimi ndimi Bwana.

  15. Walawi 19:31takriban 1490 KK

    “ ‘Msiende kwa waaguzi, wala msitafute wapunga pepo, kwa maana watawanajisi. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

  16. Walawi 19:32takriban 1490 KK

    “ ‘Uwapo mbele ya mzee, simama ili kuonyesha heshima kwa wazee, nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.

  17. Walawi 19:33takriban 1490 KK

    “ ‘Wakati mgeni anaishi pamoja nawe katika nchi yako, usimnyanyase.

  18. Walawi 19:34takriban 1490 KK

    Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

  19. Walawi 19:35takriban 1490 KK

    “ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi.

  20. Walawi 19:36takriban 1490 KK

    Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efa halali, na hini halali. Mimi ndimi Bwana Mungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri.

  21. Walawi 19:37takriban 1490 KK

    “ ‘Shika amri zangu zote na sheria zangu zote, nawe uzifuate. Mimi ndimi Bwana.’ ”

  22. Walawi 20:1takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  23. Walawi 20:2takriban 1490 KK

    “Sema na wana wa Israeli: ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi katika Israeli ambaye atamtoa yeyote miongoni mwa watoto wake kuwa sadaka kwa mungu Moleki, mtu huyo lazima auawe. Watu wa jumuiya hiyo watampiga kwa mawe.

  24. Walawi 20:3takriban 1490 KK

    Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake. Kwa maana kwa kumtoa mmoja wa watoto wake kwa mungu Moleki, amenajisi madhabahu yangu na kulinajisi Jina langu takatifu.

  25. Walawi 20:4takriban 1490 KK

    Ikiwa watu wa jumuiya watafumba macho wakati mtu huyo anapomtoa mmoja wa watoto wake kwa mungu Moleki, nao wakaacha kumuua,