Reuel
Mistari inayomtaja Reuel
Ada akamzalia Esau Elifazi, Basemathi akamzaa Reueli,
Haya ndiyo majina ya wana wa Esau: Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia.
Wana wa Reueli ni: Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Basemathi mkewe Esau.
Wakuu wa wana wa Reueli, mwana wa Esau ni: Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa Reueli huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Basemathi mkewe Esau.
Wana wa Esau walikuwa: Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.
Wana wa Reueli walikuwa: Nahathi, Zera, Shama na Miza.