Skip to content

Hezron

13 mistari · 9 wanafamilia

Anajulikana pia kama: Esrom

Mistari inayomtaja Hezron

  1. Wana wa Yuda ni: Eri, Onani, Shela, Peresi na Zera (lakini Eri na Onani walifariki katika nchi ya Kanaani). Wana wa Peresi ni: Hesroni na Hamuli.

  2. Wazao wa Peresi walikuwa: kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni; kutoka kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.

  3. Hivi ndivyo vizazi vya Peresi: Peresi alimzaa Hesroni,

  4. Hesroni akamzaa Ramu, Ramu akamzaa Aminadabu,

  5. Wana wa Peresi walikuwa: Hesroni na Hamuli.

  6. Wana wa Hesroni walikuwa: Yerameeli, Ramu na Kalebu.

  7. Kalebu mwana wa Hesroni akazaa wana na mkewe Azuba (na pia na Yeriothi). Hawa ndio wana Azuba aliomzalia Kalebu: Yesheri, Shobabu na Ardoni.

  8. Hatimaye, Hesroni akakutana kimwili na binti wa Makiri babaye Gileadi (ambaye alimwoa alipokuwa na umri wa miaka sitini), naye akamzaa Segubu.

  9. Baada ya Hesroni kufa huko Efrathi, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa.

  10. Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa: Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya.

  11. Wana wa Yuda walikuwa: Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali.

  12. Yuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari, Peresi akamzaa Hesroni, Hesroni akamzaa Aramu,

  13. Nashoni alikuwa mwana wa Aminadabu, Aminadabu alikuwa mwana wa Aramu, Aramu alikuwa mwana wa Hesroni, Hesroni alikuwa mwana wa Peresi, Peresi alikuwa mwana wa Yuda,