Skip to content
Zaburi 118:7-21

Zaburi 118:7-21

7
Bwana yuko pamoja nami, yeye ni msaidizi wangu. Nitawatazama adui zangu wakiwa wameshindwa.
8
Ni bora kumkimbilia Bwana kuliko kumtumainia mwanadamu.
9
Ni bora kumkimbilia Bwana kuliko kuwatumainia wakuu.
10
Mataifa yote yalinizunguka, lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
11
Walinizunguka pande zote, lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
12
Walinizunguka kama kundi la nyuki, lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo; kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
13
Nilisukumwa nyuma karibu kuanguka, lakini Bwana alinisaidia.
14
Bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu, yeye amefanyika wokovu wangu.
15
Sauti za shangwe na ushindi zinavuma hemani mwa wenye haki: “Mkono wa kuume wa Bwana umetenda mambo makuu!
16
Mkono wa kuume wa Bwana umeinuliwa juu, mkono wa kuume wa Bwana umetenda mambo makuu!”
17
Sitakufa, bali nitaishi, nami nitatangaza yale Bwana aliyoyatenda.
18
Bwana ameniadhibu vikali, lakini hakuniacha nife.
19
Nifungulie malango ya haki, nami nitaingia na kumshukuru Bwana.
20
Hili ni lango la Bwana ambalo wenye haki wanaweza kuliingia.
21
Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu, umekuwa wokovu wangu.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options