Skip to content
1 Nyakati 6:54-81

1 Nyakati 6:54-81

54
Zifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao (walipewa wazao wa Aroni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):
55
Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na sehemu ya malisho inayouzunguka.
56
Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.
57
Kwa hiyo wazao wa Aroni walipewa miji ifuatayo pamoja na eneo la malisho: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa,
58
Hileni, Debiri,
59
Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho.
60
Kutoka kabila la Benyamini walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho. Miji hii kumi na mitatu iligawanywa miongoni mwa koo za Wakohathi.
61
Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase.
62
Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.
63
Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.
64
Kwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yake ya malisho.
65
Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu.
66
Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu.
67
Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri,
68
Yokmeamu, Beth-Horoni,
69
Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo yake ya malisho.
70
Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki miji ya Aneri na Bileamu pamoja na maeneo yake ya malisho.
71
Wagershoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho: Katika nusu ya kabila la Manase: walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi.
72
Kutoka kabila la Isakari walipokea Kedeshi, Daberathi,
73
Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo yake ya malisho.
74
Kutoka kabila la Asheri walipokea Mashali, Abdoni,
75
Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo yake ya malisho.
76
Kutoka kabila la Naftali walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu pamoja na maeneo yake ya malisho.
77
Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo: kutoka kabila la Zabuloni walipokea Yokneamu, Karta, Rimoni na Tabori pamoja na maeneo yake ya malisho.
78
Kutoka kabila la Reubeni, ngʼambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahasa,
79
Kedemothi na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho.
80
Na kutoka kabila la Gadi walipokea Ramothi huko Gileadi, Mahanaimu,
81
Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo yake ya malisho.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options