Skip to content
1 Nyakati 7:1-5

Wazao wa Isakari

1 Nyakati 7:1-5
1
Wana wa Isakari walikuwa: Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne.
2
Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600.
3
Mwana wa Uzi alikuwa: Izrahia. Wana wa Izrahia walikuwa: Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao.
4
Kulingana na ukoo wa jamaa zao, walikuwa na watu hodari wa vita wapatao 36,000, kwa sababu walikuwa na wanawake na watoto wengi.
5
Jamaa ya watu waliokuwa wapiganaji hodari kutoka koo zote za Isakari, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, jumla yao walikuwa 87,000.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options