Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Serpent: Venom of

9 mistari · 16 vipengele

Mistari kuhusu Venom of

  1. Nitatuma njaa kali dhidi yao maradhi mabaya, yateketezayo na tauni ya kufisha; nitawapelekea meno makali ya wanyama mwitu, na sumu ya nyoka wale watambaao mavumbini.

  2. Mvinyo wao ni sumu ya nyoka, sumu yenye kufisha ya swila.

  3. Atanyonya sumu za majoka; meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua.

  4. Sumu yao ni kama sumu ya nyoka, kama ile ya fira ambaye ameziba masikio yake,

  5. Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka, sumu ya nyoka iko midomoni mwao.

  6. Usiukodolee macho mvinyo wakati ukiwa mwekundu, wakati unapometameta kwenye bilauri, wakati ushukapo taratibu!

  7. Mwishowe huuma kama nyoka na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu.

  8. Lakini Paulo akamkungʼutia yule nyoka ndani ya moto wala yeye hakupata madhara yoyote.

  9. Watu walikuwa wanangoja avimbe au aanguke ghafula na kufa. Lakini baada ya kungoja kwa muda mrefu na kuona kwamba hakuna chochote kisicho cha kawaida kilichomtokea, wakabadili mawazo yao na kuanza kusema kwamba yeye ni mungu.