Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Reptiles

37 mistari · 21 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mungu akasema, “Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo ardhini na wanyama pori, kila mnyama kulingana na aina yake.” Ikawa hivyo.

  2. Mungu akafanya wanyama pori kulingana na aina zake, wanyama wa kufugwa kulingana na aina zake, na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi kulingana na aina zake. Mungu akaona kuwa hili ni jema.

  3. Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote watambaao juu ya nchi.”

  4. Kama ukikataa kuwaruhusu kuondoka, basi nitaipiga nchi yako yote kwa kuwaletea vyura.

  5. “ ‘Kuhusu wanyama watambaao juu ya ardhi, hawa ni najisi kwenu: kicheche, panya, aina yoyote ya mijusi mikubwa,

  6. guruguru, kenge, mijusi ya ukutani, goromoe na kinyonga.

  7. Hao wote watambaao juu ya ardhi ni najisi kwenu. Yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni.

  8. Yeyote atakayekula sehemu ya mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Yeyote atakayebeba mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni.

  9. “ ‘Kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi ni chukizo; kisiliwe.

  10. Msile kiumbe chochote kitambaacho juu ya ardhi, kiwe kitambaacho kwa tumbo lake, au kitambaacho kwa miguu minne au kwa miguu mingi; ni chukizo.

  11. Msijitie unajisi kwa chochote katika viumbe hivi. Msijitie unajisi kwa viumbe hivyo au kutiwa unajisi navyo.

  12. ili msije mkajichafua na kujitengenezea sanamu au kinyago chenye umbo lolote kama la mwanaume au mwanamke,

  13. au kama kiumbe kitambaacho juu ya ardhi au samaki yeyote aliye ndani ya maji.

  14. Aliwaongoza kupitia jangwa lile kubwa na la kutisha, nchi ile ya kiu isiyo na maji, yenye nyoka wa sumu na nge. Aliwatolea maji kutoka kwenye mwamba mgumu.

  15. Mvinyo wao ni sumu ya nyoka, sumu yenye kufisha ya swila.

  16. Akaelezea maisha ya mimea kuanzia mwerezi wa Lebanoni hadi hisopo iotayo ukutani. Pia akafundisha kuhusu wanyama na ndege, wanyama wenye damu baridi, wakiwemo samaki.

  17. Aliisafisha anga kwa pumzi yake; kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.

  18. Nimekuwa ndugu wa mbweha, rafiki wa mabundi.

  19. Sumu yao ni kama sumu ya nyoka, kama ile ya fira ambaye ameziba masikio yake,

  20. Kama konokono ayeyukavyo akitembea, kama mtoto aliyezaliwa akiwa mfu, wasilione jua.

  21. Utawakanyaga simba na nyoka wakali, simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu.

  22. wanyama wa mwituni na mifugo yote, viumbe vidogo na ndege warukao,

  23. Mwishowe huuma kama nyoka na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu.

  24. “Mruba anao binti wawili waliao, ‘Nipe! Nipe!’ “Kuna vitu vitatu visivyotosheka kamwe, naam, viko vinne visivyosema, ‘Yatosha!’:

  25. Mtoto mchanga atacheza karibu na shimo la nyoka, naye mtoto mdogo ataweka mkono wake kwenye kiota cha fira.