Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Pontius Pilate: Allows Joseph of Arimathaea to take Jesus' body

7 mistari · 4 vipengele

Mistari kuhusu Allows Joseph of Arimathaea to take Jesus' body

  1. Ilipofika jioni, alifika mtu mmoja tajiri kutoka Arimathaya aitwaye Yosefu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.

  2. Akamwendea Pilato ili kumwomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe.

  3. Yosefu wa Arimathaya, mtu aliyeheshimiwa katika Baraza, na ambaye alikuwa anautarajia Ufalme wa Mungu, akamwendea Pilato kwa ujasiri na kumwomba mwili wa Yesu.

  4. Pilato alikuwa akijiuliza kama Yesu alikuwa amekwisha kufa. Hivyo akamwita yule jemadari, akamuuliza iwapo Yesu alikuwa amekwisha kufa.

  5. Baada ya kupata habari kutoka kwa yule jemadari kwamba kweli amekwisha kufa, Pilato akampa Yosefu ruhusa ya kuuchukua huo mwili.

  6. Yosefu alikwenda kwa Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu.

  7. Baada ya mambo haya, Yosefu wa Arimathaya, aliyekuwa mfuasi wa Yesu, ingawa kwa siri kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi, alimwomba Pilato ruhusa ili kuuchukua mwili wa Yesu. Pilato alimruhusu, hivyo akaja, akauchukua.