Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Personal Call

13 mistari · 30 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Siku baada ya siku zinatoa habari, usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa.

  2. Hakuna msemo wala lugha, ambapo sauti zao hazisikiki.

  3. kando ya malango yaelekeayo mjini, kwenye maingilio, hulia kwa sauti kubwa, akisema:

  4. “Ni ninyi wanaume, ninaowaita; ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote.

  5. hivyo inawapasa kuwatii na kufanya kila kitu wanachowaambia. Lakini msifuate yale wanayotenda, kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri.

  6. Wao hufunga mizigo mikubwa na kuiweka mabegani mwa watu, lakini wao wenyewe hawako radhi hata kuinua kidole ili kuisogeza.

  7. “Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao.

  8. Wanapenda kukalia viti vya heshima katika karamu, na vile viti maalum sana katika masinagogi.

  9. Hupenda kusalimiwa masokoni na kutaka watu wawaite ‘Rabi.’

  10. “Lakini ninyi msiitwe ‘Rabi,’ kwa sababu mnaye Bwana mmoja na ninyi nyote ni ndugu.

  11. Nanyi msimwite mtu yeyote ‘Baba,’ hapa duniani, kwa maana mnaye Baba mmoja, naye yuko mbinguni.

  12. Iweje basi, kama yeye alitenda hivi ili kufanya wingi wa utukufu wake ujulikane kwa vile vyombo vya rehema yake, alivyotangulia kuvitengeneza kwa ajili ya utukufu wake,

  13. yaani pamoja na sisi, ambao pia alituita, si kutoka kwa Wayahudi peke yao, bali pia kutoka kwa watu wa Mataifa?