Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Modern Samaria

59 mistari · 23 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Filipo akateremkia mji mmoja wa Samaria akawahubiria habari za Kristo

  2. Watu walipomsikia Filipo na kuona ishara na miujiza aliyofanya, wakasikiliza kwa bidii yale aliyosema.

  3. Pepo wachafu wakawa wakiwatoka watu wengi huku wakipiga kelele na wengi waliopooza na viwete wakaponywa.

  4. Hivyo pakawa na furaha kuu katika mji huo.

  5. Basi mtu mmoja jina lake Simoni alikuwa amefanya uchawi kwa muda mrefu katika mji huo akiwashangaza watu wote wa Samaria. Alijitapa kwamba yeye ni mtu mkuu,

  6. nao watu wote wakubwa kwa wadogo wakamsikiliza na kumaka, wakisema “Mtu huyu ndiye uweza wa Mungu ujulikanao kama ‘Uweza Mkuu.’ ”

  7. Wakamfuata kwa sababu kwa muda mrefu alikuwa amewashangaza kwa uchawi wake.

  8. Ndipo kanisa katika Uyahudi wote, Galilaya na Samaria likafurahia wakati wa amani. Likatiwa nguvu, na kwa faraja ya Roho Mtakatifu, idadi yake ikazidi kuongezeka, na likaendelea kudumu katika kumcha Bwana.

  9. Hivyo askari, kwa kufuata maelekezo waliyopewa, wakamchukua Paulo wakati wa usiku na kumleta mpaka Antipatri.