Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Leviathan

34 mistari · 8 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Upanga unaomfikia haumdhuru, wala mkuki au mshale wala fumo.

  2. Chuma hukiona kama unyasi, na shaba kama mti uliooza.

  3. Mishale haimfanyi yeye akimbie; mawe ya kombeo kwake ni kama makapi.

  4. Rungu kwake huwa kama kipande cha jani kavu; hucheka sauti za kugongana kwa mkuki.

  5. Sehemu zake za chini kwenye tumbo zina menomeno na mapengo kama vigae vya chungu, zikiacha mburuzo kwenye matope kama chombo chenye meno cha kupuria.

  6. Huvisukasuka vilindi kama sufuria kubwa ichemkayo, na kukoroga bahari kama chungu cha marhamu.

  7. Anapopita nyuma yake huacha mkondo unaometameta; mtu angedhani vilindi vilikuwa na mvi.

  8. Hakuna chochote duniani kinacholingana naye: yeye ni kiumbe kisicho na woga.

  9. Yeye huwatazama chini wale wote wenye kujivuna; yeye ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.”