Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Joy: Unclassified scriptures relating to

59 mistari · 91 vipengele

Mistari kuhusu Unclassified scriptures relating to

Chuja kwa kitabu
  1. Bwana umeniwekea fungu langu na kikombe changu; umeyafanya mambo yangu yote yawe salama.

  2. Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri, hakika nimepata urithi mzuri.

  3. Nimemweka Bwana mbele yangu daima. Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, sitatikisika.

  4. Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao utapumzika salama,

  5. Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe,

  6. ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele.

  7. Zaburi ya Daudi. Funzo. Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake, ambaye dhambi zake zimefunikwa.

  8. Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi, na ambaye rohoni mwake hamna udanganyifu.

  9. Nafsi yangu itatoshelezwa kama kwa wingi wa vyakula; kwa midomo iimbayo kinywa changu kitakusifu wewe.

  10. Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe, ninawaza juu yako makesha yote ya usiku.

  11. Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu, chini ya uvuli wa mbawa zako naimba.

  12. Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe, wanaotembea katika mwanga wa uwepo wako, Ee Bwana.

  13. Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa, wanafurahi katika haki yako.

  14. Nuru huangaza wenye haki na furaha kwa watu wanyofu wa moyo.

  15. Furahini katika Bwana, ninyi mlio wenye haki, lisifuni jina lake takatifu.

  16. Zaburi ya shukrani. Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote.

  17. Mwabuduni Bwana kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.

  18. Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika sheria ya Bwana.

  19. Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wao wote.

  20. Wapandao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe.

  21. Yeye azichukuaye mbegu zake kwenda kupanda, huku akilia, atarudi kwa nyimbo za shangwe, akichukua miganda ya mavuno yake.

  22. Katika siku ile utasema: “Nitakusifu wewe, Ee Bwana. Ingawa ulinikasirikia, hasira yako imegeukia mbali nawe umenifariji.

  23. Hakika Mungu ni wokovu wangu; nitamtumaini wala sitaogopa. Bwana, Bwana, ni nguvu zangu na wimbo wangu; amekuwa wokovu wangu.”

  24. Kwa furaha mtachota maji kutoka visima vya wokovu.

  25. Katika siku hiyo mtasema: “Mshukuruni Bwana, mliitie jina lake; julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya, tangazeni kuwa jina lake limetukuka.