Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Hatred: Scriptures relating to

15 mistari · 40 vipengele

Mistari kuhusu Scriptures relating to

  1. Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake, lakini moyoni mwake huficha udanganyifu.

  2. Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini, kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake.

  3. Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu, lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko.

  4. “Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Mpende jirani yako na umchukie adui yako.’

  5. Lakini ninawaambia: Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi,

  6. “Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba ulinichukia mimi kabla yenu.

  7. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeliwapenda kama vile unavyowapenda walio wake. Kwa sababu ninyi si wa ulimwengu, lakini mimi nimewachagua kutoka ulimwengu, hii ndiyo sababu ulimwengu unawachukia.

  8. Yeyote anayenichukia mimi, anamchukia pia na Baba yangu.

  9. Kama sikuwa nimefanya miujiza ambayo haijapata kufanywa na mtu mwingine yeyote, wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa wameiona miujiza hii na bado wakatuchukia mimi na Baba yangu.

  10. Lakini hii ni kutimiza lile neno lililoandikwa kwenye Sheria kwamba, ‘Walinichukia pasipo sababu.’

  11. Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi,

  12. kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

  13. Ndugu zangu, ninyi msistaajabu kama ulimwengu ukiwachukia.

  14. Sisi tunajua ya kwamba tumepita mautini kuingia uzimani, kwa sababu tunawapenda ndugu. Kila asiyempenda ndugu yake akaa mautini.

  15. Yeyote amchukiaye ndugu yake ni muuaji, nanyi mwajua ya kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake.