Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Ablution: Of the hands

7 mistari · 10 vipengele

Mistari kuhusu Of the hands

  1. “Tengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kwa ajili ya kunawia. Liweke kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, kisha uweke maji ndani yake.

  2. Aroni na wanawe watanawa mikono na miguu yao kwa maji yatokayo katika hilo sinia.

  3. Wakati wowote wanapoingia katika Hema la Kukutania, watanawa kwa maji ili kwamba wasije wakafa. Pia, wanapokaribia madhabahu ili kuhudumu kwa kuleta sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto,

  4. watanawa mikono na miguu yao ili kwamba wasije wakafa. Hii itakuwa ni amri ya kudumu kwa ajili ya Aroni na wazao wake kwa vizazi vijavyo.”

  5. Akaweka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, akaweka maji ndani yake kwa ajili ya kunawia,

  6. Naye Mose, Aroni na wanawe wakayatumia kwa kunawia mikono na miguu yao.

  7. Wakanawa kila walipoingia katika Hema la Kukutania au walipoikaribia madhabahu kama Bwana alivyomwagiza Mose.