Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Abia

9 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Samweli alipokuwa mzee, akaweka wanawe kuwa waamuzi wa Israeli.

  2. Mzaliwa wa kwanza alikuwa Yoeli, na la wa pili lilikuwa Abiya, nao wakatumika huko Beer-Sheba.

  3. Lakini wanawe hawakuenenda katika njia zake. Waliziacha wakageukia faida za udanganyifu nao wakapokea rushwa na kupotosha haki.

  4. Basi wazee wote wa Israeli wakakusanyika pamoja na kumjia Samweli huko Rama.

  5. Wakamwambia, “Wewe umekuwa mzee, nao wanao hawaenendi katika njia zako, sasa tuteulie mfalme wa kutuongoza, kama ilivyo kwa mataifa mengine yote.”

  6. Wana wa Samweli walikuwa: Yoeli mzaliwa wake wa kwanza, na Abiya mwanawe wa pili.

  7. ya saba Hakosi, ya nane Abiya,

  8. Ido, Ginethoni, Abiya,

  9. Wakati wa Herode mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zekaria, ambaye alikuwa wa ukoo wa kikuhani wa Abiya. Elizabeti mkewe alikuwa pia mzao wa Aroni.