Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kumbukumbu 1:13takriban 1451 KK

    Chagueni baadhi ya watu wenye hekima, wenye ufahamu na wanaoheshimika kutoka kila kabila lenu, nami nitawaweka juu yenu.”

  2. Kumbukumbu 1:14takriban 1451 KK

    Mlinijibu, “Shauri ulilolitoa ni zuri.”

  3. Kumbukumbu 1:15takriban 1451 KK

    Kwa hiyo niliwachukua wanaume viongozi wa makabila yenu, wenye hekima na wanaoheshimika, nami nikawateua wawe na mamlaka juu yenu kama majemadari wa maelfu, wa mamia, wa hamsini, na wa makumi, na kama maafisa wa makabila.

  4. Kumbukumbu 1:16takriban 1451 KK

    Nami wakati ule nikawaagiza waamuzi wenu: Sikilizeni magomvi kati ya ndugu zenu na mwamue kwa haki, hata kama shauri ni kati ya ndugu wa Kiisraeli, au kati ya mmoja wa ndugu wa Kiisraeli na mgeni.

  5. Kumbukumbu 1:17takriban 1451 KK

    Msionyeshe upendeleo katika maamuzi; wasikilizeni wote sawasawa, wadogo kwa wakubwa. Msimwogope mtu yeyote, kwa kuwa hukumu ni ya Mungu. Mniletee mimi shauri lolote lililo gumu sana kwenu, nami nitalisikiliza.

  6. Kumbukumbu 1:18takriban 1451 KK

    Nami wakati ule niliwaambia kila kitu ambacho mngefanya.

  7. Kumbukumbu 1:19takriban 1451 KK

    Kisha, kama Bwana Mungu wetu alivyotuamuru, tuliondoka kutoka Horebu na kwenda kuelekea nchi ya vilima ya Waamori, kupitia jangwa lile kubwa lote la kutisha, lile mliloliona, nasi tukafika Kadesh-Barnea.

  8. Kumbukumbu 1:20takriban 1451 KK

    Kisha niliwaambia, “Mmefika katika nchi ya vilima ya Waamori, ambayo Bwana Mungu wetu anatupa.

  9. Kumbukumbu 1:21takriban 1451 KK

    Tazama, Bwana Mungu wenu amewapa nchi. Pandeni mkaimiliki kama Bwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaambia. Msiogope, wala msikate tamaa.”

  10. Kumbukumbu 1:22takriban 1451 KK

    Ndipo ninyi nyote mkanijia na kusema, “Tupeleke watu watutangulie kuipeleleza nchi kwa ajili yetu, na kutuletea taarifa kuhusu njia tutakayopita, na miji tutakayoiendea.”

  11. Kumbukumbu 1:23takriban 1451 KK

    Wazo hilo lilionekana zuri kwangu; kwa hiyo niliwachagua watu wenu kumi na wawili, mwanaume mmoja kutoka kila kabila.

  12. Kumbukumbu 1:24takriban 1451 KK

    Waliondoka na kukwea katika nchi ya vilima, wakafika katika Bonde la Eshkoli na kuipeleleza.

  13. Kumbukumbu 1:25takriban 1451 KK

    Wakachukua baadhi ya matunda ya nchi, wakatuletea na kutuarifu, “Ni nchi nzuri ambayo Bwana Mungu wetu anatupa.”

  14. Kumbukumbu 1:26takriban 1451 KK

    Lakini hamkuwa tayari kukwea, mkaasi dhidi ya amri ya Bwana Mungu wenu.

  15. Kumbukumbu 1:27takriban 1451 KK

    Mkanungʼunika ndani ya mahema yenu na kusema, “Bwana anatuchukia, kwa hiyo alitutoa Misri ili kututia mikononi mwa Waamori kutuangamiza.

  16. Kumbukumbu 1:28takriban 1451 KK

    Twende wapi? Ndugu zetu wametufanya kufa moyo. Wanasema, ‘Watu wa huko wana nguvu zaidi na ni warefu kuliko sisi tulivyo; miji ni mikubwa, yenye kuta zilizofika juu angani. Zaidi ya hayo, tumewaona Waanaki huko.’ ”

  17. Kumbukumbu 1:29takriban 1451 KK

    Ndipo nikawaambia, “Msihofu, wala msiwaogope.

  18. Kumbukumbu 1:30takriban 1451 KK

    Bwana Mungu wenu anayewatangulia, atawapigania, kama alivyofanya kwa ajili yenu huko Misri, mbele ya macho yenu hasa,

  19. Kumbukumbu 1:31takriban 1451 KK

    na pia huko jangwani. Huko mliona jinsi Bwana Mungu wenu alivyowachukua, kama baba amchukuavyo mwanawe, katika njia yote mliyoiendea mpaka mkafika mahali hapa.”

  20. Kumbukumbu 1:32takriban 1451 KK

    Pamoja na hili, hamkumtegemea Bwana Mungu wenu,

  21. Kumbukumbu 1:33takriban 1451 KK

    ambaye aliwatangulia katika safari yenu, kwa moto usiku na kwa wingu mchana, kuwatafutia mahali penu pa kupiga kambi na kuwaonyesha njia mtakayoiendea.

  22. Kumbukumbu 1:34takriban 1451 KK

    Wakati Bwana aliposikia lile mlilosema, alikasirika, akaapa, akasema:

  23. Kumbukumbu 1:35takriban 1451 KK

    “Hakuna mtu wa kizazi hiki kiovu atakayeona nchi nzuri niliyoapa kuwapa baba zenu,

  24. Kumbukumbu 1:36takriban 1451 KK

    isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune. Yeye ataiona, nami nitampa yeye na wazao wake nchi aliyoikanyaga kwa miguu, kwa sababu alimfuata Bwana kwa moyo wote.”

  25. Kumbukumbu 1:37takriban 1451 KK

    Kwa sababu yenu Bwana pia alinikasirikia mimi, akasema, “Hutaingia hiyo nchi pia.