Rukia maudhui

circa 800–400 BC

The Hebrew Prophets

God speaks through Isaiah, Jeremiah, and the minor prophets—calling Israel to repentance and foretelling the coming Messiah.

3,706 mistari · 14 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Ndugu zako, watu wa jamaa yako mwenyewe: hata wao wamekusaliti; wameinua kilio kikubwa dhidi yako. Usiwaamini, ingawa wanazungumza mema juu yako.

  2. “Nitaiacha nyumba yangu, nitupe urithi wangu; nitamtia yeye nimpendaye mikononi mwa adui zake.

  3. Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba wa msituni. Huningurumia mimi, kwa hiyo ninamchukia.

  4. Je, urithi wangu haukuwa kama ndege wa mawindo wa madoadoa ambaye ndege wengine wawindao humzunguka na kumshambulia? Nenda ukawakusanye pamoja wanyama wote wa mwituni; walete ili wale.

  5. Wachungaji wengi wataliharibu shamba langu la mizabibu na kulikanyaga shamba langu; watalifanya shamba langu zuri kuwa jangwa la ukiwa.

  6. Litafanywa kuwa jangwa, lililokauka na kuachwa ukiwa mbele zangu; nchi yote itafanywa jangwa kwa sababu hakuna hata mmoja anayejali.

  7. Juu ya miinuko yote ilivyo kama jangwani mharabu atajaa, kwa maana upanga wa Bwana utawala, kuanzia ncha moja ya nchi hadi nyingine; hakuna hata mmoja atakayekuwa salama.

  8. Watapanda ngano lakini watavuna miiba; watajitaabisha lakini hawatafaidi chochote. Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako kwa sababu ya hasira kali ya Bwana Mungu.”

  9. Yeremia 12:14takriban 603 KK

    Hili ndilo asemalo Bwana: “Kwa habari ya majirani zangu wote wabaya wanaonyangʼanya urithi ambao ninawapa watu wangu Israeli, nitawangʼoa kutoka nchi zao, nami nitaingʼoa nyumba ya Yuda kutoka katikati yao.

  10. Yeremia 12:15takriban 603 KK

    Lakini baada ya kuwangʼoa, nitawahurumia tena na kumrudisha kila mmoja wao kwenye urithi wake mwenyewe na kwenye nchi yake mwenyewe.

  11. Yeremia 12:16takriban 603 KK

    Ikiwa watajifunza vyema njia za watu wangu na kuapa kwa Jina langu, wakisema, ‘Hakika kama Bwana aishivyo,’ hata kama wakati fulani walifundisha watu wangu kuapa kwa Baali, ndipo watakapofanywa imara katikati ya watu wangu.

  12. Yeremia 12:17takriban 603 KK

    Lakini kama taifa lolote halitasikiliza na kutii, nitalingʼoa kabisa na kuliangamiza,” asema Bwana.

  13. Yeremia 13:1takriban 599 KK

    Hili ndilo Bwana aliloniambia: “Nenda ununue mkanda wa kitani, ujivike kiunoni mwako, lakini usiuache uguse maji.”

  14. Yeremia 13:2takriban 599 KK

    Kwa hiyo nikanunua mkanda, kama Bwana alivyoniagiza, nikajivika kiunoni.

  15. Yeremia 13:3takriban 599 KK

    Ndipo neno la Bwana likanijia kwa mara ya pili:

  16. Yeremia 13:4takriban 599 KK

    “Chukua mkanda ulionunua ambao umeuvaa kiunoni mwako, uende sasa Frati uufiche ndani ya ufa mdogo kwenye mwamba.”

  17. Yeremia 13:5takriban 599 KK

    Ndipo nikaenda na kuuficha ule mkanda huko Frati, kama Bwana alivyoniamuru.

  18. Yeremia 13:6takriban 599 KK

    Baada ya siku nyingi Bwana akaniambia, “Nenda sasa Frati ukauchukue ule mkanda niliokuambia uufiche huko.”

  19. Yeremia 13:7takriban 599 KK

    Hivyo nikaenda Frati na kuuchimbua ule mkanda kutoka pale nilipokuwa nimeuficha, lakini sasa ulikuwa umeharibika na haufai tena kabisa.

  20. Yeremia 13:8takriban 599 KK

    Ndipo neno la Bwana likanijia:

  21. Yeremia 13:9takriban 599 KK

    “Hili ndilo Bwana asemalo: ‘Vivyo hivyo ndivyo nitakavyokiharibu kiburi cha Yuda na kiburi kikuu cha Yerusalemu.

  22. Yeremia 13:10takriban 599 KK

    Watu hawa waovu, wanaokataa kusikiliza maneno yangu, wafuatao ukaidi wa mioyo yao na kufuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu, watakuwa kama mkanda huu ambao haufai kabisa!

  23. Yeremia 13:11takriban 599 KK

    Kwa maana kama vile mkanda ufungwavyo kiunoni mwa mtu, ndivyo nilivyojifunga nyumba yote ya Israeli na nyumba yote ya Yuda,’ asema Bwana, ‘ili wawe watu wangu kwa ajili ya utukufu wangu, sifa na heshima yangu. Lakini hawajasikiliza.’

  24. Yeremia 13:12takriban 599 KK

    “Waambie: ‘Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: kila kiriba inapasa kijazwe mvinyo.’ Kama wao wakikuambia, ‘Kwani hatujui kwamba kila kiriba inapasa kijazwe mvinyo?’

  25. Yeremia 13:13takriban 599 KK

    Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: nitawajaza ulevi wote waishio katika nchi hii, pamoja na wafalme waketio juu ya kiti cha enzi cha Daudi, makuhani, manabii na wale wote waishio Yerusalemu.