God
Mistari inayomtaja God
unampa utulivu siku za shida, mpaka shimo litakapokuwa limechimbwa kwa ajili ya mwovu.
Kwa kuwa Bwana hatawakataa watu wake, hatauacha urithi wake.
Kama Bwana asingelinisaidia upesi, ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo.
Niliposema, “Mguu wangu unateleza,” Ee Bwana, upendo wako ulinishikilia.
Wakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu, faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu.
Je, kiti cha utawala wa udhalimu kitajiunga nawe, ule utawala uletao taabu kutokana na sheria zake?
Lakini Bwana amekuwa ngome yangu, na Mungu wangu amekuwa mwamba ninaoukimbilia.
Yeye atawalipa kwa ajili ya dhambi zao na atawaangamiza kwa ajili ya maovu yao; Bwana Mungu wetu atawaangamiza.
Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu.
Tuje mbele zake kwa shukrani, tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.
Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, mfalme mkuu juu ya miungu yote.
Mkononi mwake mna vilindi vya dunia, na vilele vya milima ni mali yake.
Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya, na mikono yake iliumba nchi kavu.
Njooni, tusujudu, tumwabudu, tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu,
kwa maana yeye ndiye Mungu wetu, na sisi ni watu wa malisho yake, kondoo chini ya utunzaji wake. Kama mkiisikia sauti yake leo,
ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima, ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu.
Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile, nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka, nao hawajazijua njia zangu.”
Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu, “Kamwe hawataingia rahani mwangu.”
Mwimbieni Bwana wimbo mpya; mwimbieni Bwana dunia yote.
Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.
Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.
Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.
Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini Bwana aliziumba mbingu.
Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.
Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa, mpeni Bwana utukufu na nguvu.