Mithali 5:9-21
9
usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine na miaka yako kwa aliye mkatili,
10
wageni wasije wakasherehekea utajiri wako na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya mwanaume mwingine.
11
Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, wakati nyama na mwili wako vimechakaa.
12
Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!
13
Sikuwatii walimu wangu wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.
14
Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa katikati ya kusanyiko lote.”
15
Kunywa maji kutoka kwenye kisima chako mwenyewe, maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe.
16
Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani?
17
Na viwe vyako mwenyewe, kamwe visishirikishwe wageni.
18
Chemchemi yako na ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako.
19
Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri: matiti yake na yakutosheleze siku zote, nawe utekwe daima na upendo wake.
20
Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba? Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine?
21
Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana, naye huyapima mapito yake yote.
Settings