Skip to content
Mwanzo 36:20-30

Mwanzo 36:20-30

20
Hawa ndio walikuwa wana wa Seiri, Mhori, waliokuwa wakiishi katika nchi ile: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,
21
Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori.
22
Wana wa Lotani walikuwa: Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani.
23
Wana wa Shobali walikuwa: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
24
Wana wa Sibeoni walikuwa: Aiya na Ana. Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda za Sibeoni baba yake.
25
Watoto wa Ana walikuwa: Dishoni na Oholibama binti wa Ana.
26
Wana wa Dishoni walikuwa: Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
27
Wana wa Eseri walikuwa: Bilhani, Zaavani na Akani.
28
Wana wa Dishani walikuwa: Usi na Arani.
29
Hawa ndio waliokuwa wakuu wa Wahori: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,
30
Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Wahori, kufuatana na makundi yao, katika nchi ya Seiri.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options