Mwanzo 36:31-39
31
Wafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala:
32
Bela mwana wa Beori alikuwa mfalme wa Edomu. Mji wake uliitwa Dinhaba.
33
Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
34
Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
35
Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
36
Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
37
Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati akawa mfalme baada yake.
38
Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
39
Baal-Hanani mwana wa Akbori alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.
Settings