Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Weights: Must be just

11 mistari · 19 vipengele

Mistari kuhusu Must be just

  1. “ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi.

  2. Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efa halali, na hini halali. Mimi ndimi Bwana Mungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri.

  3. Usiwe na mawe ya kupimia ya aina mbili katika mkoba wako, moja zito na jingine jepesi.

  4. Usiwe na vipimo viwili tofauti katika nyumba yako, kimoja kikubwa, kingine kidogo.

  5. Ni lazima uwe na uzito na vipimo sahihi na vya haki, ili upate kuishi maisha marefu katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako.

  6. Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu, bali vipimo sahihi ni furaha yake.

  7. Vipimo na mizani za halali hutoka kwa Bwana; mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye.

  8. Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti, Bwana huchukia vyote viwili.

  9. Bwana anachukia sana mawe ya kupimia ya udanganyifu, nazo mizani zisizo halali hazimpendezi.

  10. Je, bado nisahau, ee nyumba ya uovu, hazina yako uliyopata kwa udanganyifu na vipimo vilivyopunguka, ambavyo vimelaaniwa?

  11. Je, naweza kuhukumu kuwa mtu mwenye mizani ya udanganyifu hana hatia, aliye na mfuko wa mawe ya kupimia ya uongo?